Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Habari za Teknolojia kwa Wiki Hii Tarehe 15/04/2018

Kama ulipitwa na habari kubwa za teknolojia wiki hii basi hizi hapa
habari za teknolojia wiki hii habari za teknolojia wiki hii

Habari ya jumapili na karibu kwenye makala za wiki za teknolojia, Hapa utaweza kusoma habari zote za teknolojia zilizoshika chat kwa wiki nzima hapa Tanzania Tech. Sehemu hii itakusaidia kuweza kujua kwa haraka yote yaliyojiri kwenye ulimwengu mzima wa teknolojia kwa wiki hii, basi bila kupoteza muda twende tukangalie habari hizo.

Moja ya habari kubwa za teknolojia wiki hii ni kuhusu Mark Zuckerberg kuhojiwa na ma-senate wa marekani kuhusu matumizi ya data zinzopatikana kwenye mtandao wa Facebook. Aidha katika mkutano huo mambo mengi yaliongelewa ikiwa pamoja na jinsi data hizo zinavyotumika ikiwa pamoja na sakata zima la Cambridge Analytica. Kama ukusoma habari hii bofya hapo juu kujua zaidi.

Advertisement

Wiki hii kampuni ya Apple imezindua simu mpya ya iPhone 8 Red, Simu hizo maalum kwa jina la iPhone 8 RED zimezinduliwa kwasababu ya ushirikiano wa kampuni ya Apple na shirika la RED ambalo kama nilivyo sema awali ni shirika la kusaidia waafrika kujilinda na UKIMWI (HIV/AIDS). Mbali na hayo Apple pia imezindua kava la rangi nyekundu ambalo litakuwa maalum kwa simu ya iPhone X au iPhone 10, kava hili ni yale ya kufunika kabisa kioo kama inavyo onekana hapo chini.

Tablet hii ya HP Chromebook x2 inakuja na kioo cha inch 12.3 na pia inakuja na kibodi maalumu na vyote hivyo kwa bei rahisi kuliko ile ya iPad Pro, sasa kama unataka kibodi ya iPad Pro itakubidi kulipa zaidi tofauti na tablet hii mpya ya HP Chromebook x2. Upande mwingine tablet hiyo inakuja na processor za Kaby Lake chips ambazo ni Core m3 processor kutoka kampuni ya Intel’s. Kwa upande wa RAM tablet hii inakuja na RAM ya GB 4 ambayo inaweza kuongezewa hadi RAM ya GB 8, ukubwa wa ndani wa Tablet hii unakuja na ukubwa wa ndani wa GB 32 ambao unaweza kuongezewa na Memory Card hadi ya GB 256.

Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao ametangaza kuachia mikoba ya kuiongoza kampuni hiyo baada ya mkataba wake kufika tamani. Kutokana na hilo, Ferrao atakabidhi majukumu kwa mrithi wake, Sylvia Mulinge kuanzia Juni Mosi mwaka huu na kuhitimisha miaka mitatu ya kuiongoza kampuni hiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya wateja nchini. Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa bodi ya Vodacom, Ali Mufuruki inaeleza makabidhiano ya ofisi kati ya Ferrao na Sylivia yatafanyika kwa miezi mitatu na kukamilika rasmi Agosti 31 mwaka huu 2018.

Mtandao wa Youtube wiki hii ulikutwa na maswaibu mengine baada ya kusemekana kudukuliwa na baadhi ya video maarufu kama despacito kufutwa na baadae kurudiswa, Kwa mujibu wa ripoti kutoka mtandao wa The Verge, YouTube inadai kuwa udukuaji huo hausishwi na YouTube bali unahusisha Akaunti ya VEVO, na kwa mujibu wa msemaji wa VEVO, Tayari video zilizo dukuliwa zimesha fanikiwa kurudishwa na uchunguzi unaendelea kujua zaidi kuhusu Udukuaji huo.

Hivi karibuni wananchi wa nchini Kenya wataanza kunufaika kutokana na ushirikiano mpya kati ya kampuni ya huduma za Simu ya Safaricom na kampuni ya kupokea malipo ya mtandaoni ya PayPal, ushirikiano huo unalenga kuwezesha wananchi wa nchini humo kuweza kutuma na kupokea pesa kutoka huduma ya Safaricom ya M-Pesa kwenda PayPal na Paypal kuja kwenye Wallet ya M-Pesa.

Sehemu hii inakusaidia kuweza kuchukua picha ya sura yako vizuri na huku kwa nyuma kukiwa hakuonekani vizuri, yaani kunakuwa na ukungu flani au kwa kitaalam (blur). Sasa sehemu hiyo mpya ya Focus kwenye Instagram itakusaidia kuweza kupiga picha za aina hiyo, ambazo zitakuwa zina angalia zaidi sura yako kuliko sehemu nyingine za mazingira ya mahali unapo piga picha.

Simu hii ambayo imezinduliwa wiki hii huko nchini india kupitia Tovuti ya Samsung, inakuja na maboresho mapya na kamera mbili kwa nyuma kwa mara ya kwanza kwenye simu za Galaxy J7. Mbali na maboresho ya kamera, simu hii ya Galaxy J7 Duo (2018), sasa inakuja na kioo kikubwa cha inch 5.5 ambacho kinakuja na teknolojia ya Super AMOLED na HD kikiwa na uwezo wa kuonyesha rangi za tofauti hadi rangi milioni 16.

Kwa mujibu wa ripoti za baadhi ya wateja wa kulipia wa G-suite, Google ilituma barua pepe za kuwajulisha wateja wake hao kuhusu mabadiliko hayo ambayo yana tegemewa kuja kwa watumiaji wa tovuti ya Gmail kwenye siku za karibuni. Hata hivyo inasemekana kuwa Google imeanza kuruhusu baadhi ya wateja wake wa G-Suite kujaribu muonekano huo ambao unasemekana kuwa ni muonekano bora zaidi.

Kampuni ya Huawei bado inaendeleza harakati za kuhakikisha watumiaji wake wanapata simu za nzuri na za bei nafuu, kuonyesha hilo hivi leo kampuni hiyo imezindua simu nyingine ya Huawei Y6 (2018). Simu hii inakuja na maboresho mengi ikiwa pamoja na kioo cha kisasa chenye teknolojia ya Full Display.

Kama wewe ni mpenzi wa kucheza Game kupitia simu, basi ni vyema ukaifahamu simu mpya kutoka Xiaomi inayoitwa Black Shark. Hii ni simu mpya kabisa kwa wapenzi wa kucheza Game kutoka kampuni ya Xiaomi ambayo ukweli imefanya mapinduzi makubwa sana ya teknolojia hasa kwa upande wa simu zenye uwezo mkubwa wa kutumika kucheza Game.

Na hizo ndio habari kubwa za teknolojia kwa wiki hii nzima, kama ulipitwa na habari za teknolojia kwa wiki iliyopita unaweza kusoma habari hizo hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, mpaka wiki ijayo nakutakia jumapili njema.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use