Vigezo na Masharti

Upatikanaji na utumiaji wa ‘Tanzania Tech‘ ndani na nje ya Tanzania unawezeshwa na Tanzania Tech (watumiaji wa kimataifa wa tovuti wanaweza kuona matangazo ya biashara katika kurasa kadhaa zinazotolewa na kitengo cha kibiashara cha Tanzania Tech, kwa masharti yafuatayo:

1. Kwa kutumia Tanzania Tech‘ unakubaliana na kanuni hizi, ambazo zinaanza kutumika mara tu unapoanza kuingia Tanzania Tech‘. Endapo haukubaliani na yote tafadhali usiingie, kutumia na /au kuchangia Tanzania Tech‘.

2. Tanzania Tech inaweza kubadilisha masharti haya mara kwa mara kwa hiyo ziangalie mara kwa mara. Utumiaji wako wa Tanzania Tech‘ utachukuliwa kuwa kukubaliana na masharti yaliyoongezwa au kubadilishwa. Endapo haukubaliani, unatakiwa kuacha kutumia tovuti hii. Endapo kuna mgongano wowote kati ya masharti haya na masharti yanaweza kuonekana sehemu nyingine za Tanzania Tech‘ (ikiwa ni pamoja na taratibu za kurasa) basi mapya na yanayohusika zaidi yatatumika.

Masharti ya matumizi yanaendelea: • Utumiaji wa Tanzania Tech‘ • Haki ya mali akili • Uchangiaji katika Tanzania Tech • Jamii zaTanzania Tech‘ • Kanusho na kupunguza uwajibikaji • Jumla • Wiji

Utumiaji

3. Unakubaliana kutumia Tanzania Tech‘ kwa shughuli zinazokubalika kisheria, na vyovyote vile isizuie haki, kukataza mtu yoyote kutumia na kufaidi Tanzania Tech‘.

Mambo yanayokatazwa ni pamoja na unyanyasaji au kusababisha tabu au usumbufu kwa mtu yoyote, kusambaza maudhui yenye matusi au kuvuruga mtiririko wa kawaida ndani ya Tanzania Tech‘.

Haki ya Mali Akili

4. Haki miliki zote, nembo za biashara, haki za usanifu, hateza na haki nyingine za mali akili (zilizosajiliwa na ambazo hazijasaliwa) kwenye maudhui ya Tanzania Tech‘ na maudhui yote (ikiwa ni pamoja na programu) zilizoko kwenye tovuti ambazo zitaendelea kuwa mali ya Tanzania Tech au wenye leseni wengine (ambao pia ni pamoja na watumiaji wengine).

Hauruhusiwi kunakili, kufyatua upya, kuchapisha upya, kukongoroa, kupangua, kubadilisha kihandisi, kupakua, kutuma, kutangaza, kurusha, au kutoa kwa umma, au vinginevyo kutumia maudhui ya Tanzania Tech‘ kwa jia yoyote isipokuwa kwa matumizi yako binafsi na isiwe matumizi ya kibiashara.

Pia unakubali kutokukabilina, kubadilisha au kutengeneza kazi nyingine kutokana na maelezo yoyote ya Tanzania Tech‘ isipokuwa tu kwa matumizi yako binafsi yasiyo ya kibiashara. Matumizi mengine yoyote ya maelezo ya Tanzania Tech‘ yanahitaji idhini rasmi ya Tanzania Tech kimaandishi.

5. Majina, picha na nembo zinaitambulisha Tanzania Tech, Tanzania Tech Media au pande nyingine na bidhaa zao na huduma zinalindwa na hakimiliki, haki ya kubuni, na alama za Tanzania Tech, Tanzania Tech Media na/au pande nyingine. Hakuna sehemu ya masharti haya itakayochukuliwa kama ni kutoa leseni yoyote au haki ya kutumia alama yoyote ya kibishara, haki ya kubuni au haki miliki ya Tanzania Tech, Tanzania Tech Media au upande mwingine wowote ule.

Michango kwa Tanzania Tech

6. Kwa kubadilishana mchango wowote (ikijumuisha maandishi yoyote yale, picha, michoro, picha za sinema au sauti) na Tanzania Tech, unaridhia kuipa Tanzania Tech, pasipo malipo, idhini ya kutumia mchango huo kwa namna yoyote ile inavyotaka (ikijumuisha kurekebisha na kubadili mchango huo kwa sababu za kiutendaji na kiuhariri) kwa ajili ya huduma za Tanzania Tech katika chombo chochote kile cha habari ulimwenguni kote (ikijumuisha katika tovuti ya Tanzania Tech inayopatikana kwa watumiaji wa kimataifa). Katika mazingira mengine Tanzania Tech huenda ikabadilishana mchango wako na watu wengine au pande nyingine zinazoaminika.

7. Hakimiliki katika mchango wako itabakia kuwa yako na idhini hii si ya kipekee, hivyo unaweza kuendelea kutumia mchango huo katika namna yoyote ile ikiwemo kuruhusu wengine kuutumia.

8. Ili Tanzania Tech iweze kutumia mchango wako, unathibitisha kuwa mchango wako ni kazi halisi yako mwenyewe, haidhalilishi na haikiuki sheria zozote za Uingereza, kwamba unahaki ya kuipa Tanzania Tech idhini ya kutumia mchango huo kwa madhumuni maalum yaliyotajwa hapo juu, na kwamba una ridhaa ya mtu yeyote yule anayeweza kutambulika katika mchango wako au ridhaa ya mzazi wao au mlezi iwapo wana umri wa chini ya miaka 16.

9.Kwa kawaida tunaonyesha jina lako sambamba na mchango wako, labda uwe umeomba vinginevyo, lakini kwa sababu za kiutendaji wakati mwingine haiwezekani kutekeleza ombi lako. Tanzania Tech huenda ikahitaji kuwasiliana na wewe kwa madhumuni ya kiutawala na uhakiki kuhusiana na mchango wako au kuhusiana na miradi maalum. Kwa maelezo yote ya wakati na jinsi gani tunaweza kuwasiliana nawe tafadhali angalia [Sera ya Faragha ya Tanzania Tech] pamoja na masharti yoyote yale katika nchi husika pale yanapohitajika.

10.Tafadhali usijihatarishe wewe mwenyewe au wengine, kuchukua hatari yoyote ile isiyo na ulazima au kuvunja sheria yoyote ile wakati unaandaa mchango wako ambao huenda ukabadilishana na Tanzania Tech.

Hakimiliki

* Haki miliki zote, alama za biashara, haki za kubuni na haki nyingine zote za kazi za ubunifu (zilizosajiliwa au kutosajiliwa) ndani na katika Tanzania Tech‘ na maelezo yote (ikijumuisha matumizi yote) yaliyowekwa katika tovuti vitabakia kuwa chini ya Tanzania Tech na au waliopewa kibali cha leseni na Tanzania Tech (ikijumuisha watumiaji wengine). Huruhusiwi kunakili, kutoa nakala, kuchapisha upya, kupangua, kuunda upya, kupakua, kutuma, kutangaza, kusambaza, kuwezesha kupatikana kwa umma au vinginevyo kutumia maelezo ya Tanzania Tech‘ kwa namna ambayo ni nje ya matumizi yako binafsi, yasiyolenga kibiashara. Pia unakubali kutokukabilina, kubadilisha au kutengeneza kazi nyingine kutokana na maelezo yoyote ya Tanzania Tech‘ isipokuwa tu kwa matumizi yako binafsi yasiyo ya kibiashara. Matumizi mengine yoyote ya maelezo ya Tanzania Tech‘ yanahitaji idhini rasmi ya Tanzania Tech kimaandishi.

* Majina, picha na nembo zinaitambulisha Tanzania Tech, Tanzania Tech Media au pande nyingine na bidhaa zao na huduma zinalindwa na hakimiliki, haki ya kubuni, na alama za Tanzania Tech, Tanzania Tech Media na/au pande nyingine. Hakuna sehemu ya masharti haya itakayochukuliwa kama ni kutoa leseni yoyote au haki ya kutumia alama yoyote ya kibishara, haki ya kubuni au haki miliki ya Tanzania Tech, Tanzania Tech Media au upande mwingine wowote ule.

Iwapo hutaki kutoa ruhusa kwa Tanzania Tech kulingana na masharti yaliyotajwa hapo juu, tafadhali usiwasilishe au kubadilishana mchango wako kwa, au na Tanzania Tech‘.

11. Katika tukio la mchango unaohusiana na habari tafadhali kumbuka hapa huenda ikabadilishana na washirika wa Tanzania Tech  haya ni mashirika ya utangazaji yanayoheshimika ambayo hayaruhusiwi kubadili maelezo kwa namna yoyote ile au kuyatoa kwa mashirika mengine ya utangazaji ya Tanzania au ya uchapishaji.

12. Iwapo una maswali yoyote yale kuhusu maelezo ya mchango unaotolewa kwa Tanzania Tech, tafadhali angalia [Maelezo Yanayotokana na Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara na Watumiaji]

* Ili kushiriki na kutoa mchango katika sehemu zilizochaguliwa za kijamii katika Tanzania Tech‘ (ikiwemo ubao wa ujumbe na blogs) huenda ukahitajika kujisajili. Maelezo yoyote yale ya kibinafsi yanayotolewa kwa Tanzania Tech‘ kama sehemu ya mchakato wa usajili huu au mwiingiliano wowote ule na Tanzania Tech‘ yatachukuliwa, kuhifadhiwa na kutumiwa kulingana na sera ya faragha ya Tanzania Tech. [Privacy Policy].

Kanuni za Jumuiya

* Unakubali kushiriki katika jumuiya zilizopendekezwa za Tanzania Tech‘ kulinga na Kanuni za Jumuiya za Tanzania Tech zilizoorodheshwa hapa chini:

1. Kuhusu michango yako: • Michango ni lazima iwe ya kiistaarbu na yenye mvuto. • Mwenendo wa usumbufu, kuchukiza au matusi hauruhusiwi: michango lazima iwe ya kujenga na yenye heshima, isiwe na lengo baya au iliyotolewa kwa kusudi la kusababisha kero. • Mchango ulio kinyume cha sheria hauruhusiwi: michango iliyo kinyume cha sheria, usumbufu, udhalilishaji, unyanyasaji, vitisho, kudhuru, matusi, yenye lengo la kimapenzi, ubaguzi wa rangi au vinginevyo haikubaliki. • Uwe mvumilivu: Watumiaji wa rika zote na uwezo huenda wakaweza kushiriki katika jumuiya husika za Tanzania Tech community. • Michango iliyo nje ya mada au yenye lengo la kudhuru hairuhusiwi: haturuhusu kuwasilisha mchango ambao umeshatumika au unaofanana sana mara nyingi. Tafadhali usiwasilsilishe mchango wako kwa mara ya pili kwa zaidi ya mjadala mmoja au kuchangia maelezo yaliyo nje ya mada katika maeneo maalum. • Hairuhusiwi matangazo au kujitangaza.

• Michango iliyo katika lugha nyingine zaidi ya (lugha yako mfano Kiswahili) huenda ikaondolewa isipokuwa pale imeruhusiwa katika sheria za eneo au nchi husika.

• Hairuhusiwi kujiigiza kuwa mtu mwingine. • Hairuhusiwi majina yasiyolubalika. (mfano yenye kuchukiza) • URLs (anuani za tovuti) zinaweza tu kutumwa au kuwasilishwa iwapo imeruhusiwa na katika kanuni zozote zile za shirika husika. • Kutumia vibaya kwa makusudi sehemu ya kuwasilisha malalamiko hairuhusiwi. Iwapo utaendelea kufanya hivyo, hatua itachukuliwa dhidi ya akaunti yako.

Akaunti yako ya Tanzania Tech:

Iwapo unatumia logins zaidi ya moja kwa lengo la kuivuruga jumuiya au kuwaudhi watumiaji wengine, huenda ukachukuliwa hatua dhidi ya akaunti zako zote. Akaunti zote lazima zisajilliwe na anwani binafsi ya barua pepe iliyo sahihi ambayo unaitumia mara kwa mara ili barua pepe (emails) ziweze kutumwa kwako.Akaunti zilizosajiliwa kwa kutumia anwani ya barua pepe ya mtu mwingine, au anwani ya barua pepe ya muda huenda zikafungwa pasipo kutolewa taarifa. Huenda tukahitaji watumiaji wathibitishe tena akaunti zao iwapo tunaamini kuwa wamekuwa wakitumia anwani ya barua pepe siyo sahihi. Tanzania Tech ina haki ya kuzifunga akaunti iwapo mtumiaji yeyote anaonekana kuwa anatumia wakala IPS (Internet Protocol addresses) ili kujaribu kuficha matumizi ya akauti za Tanzania Tech zaidi ya moja, au iwapo mtumiaji asiyemkazi wa Tanzania anajifanya kuwa ni mtumiajai wa Tanzania, au kuvuruga huduma zetu kwa namna yoyote ile.

Usalama:

Tunashauri kuwa kamwe usitoe maelezo binasi kuhusu wewe mwenyewe au mtu mwingine yeyote yule moja kwa moja kwa umma katika jumuiya yoyote ile ya Tanzania Tech.

Mahitaji ya Kisheria:

Usiwasilishe au kubadilidhana mchango wowote wa kudhalilisha au ulio kinyume cha sheria kwa namna yoyote ile katika jumuiya za Tanzania Tech‘ . Hii inajumuisha maandishi, graphics, picha za sinema, vipindi au sauti.

• Maelezo ya mchango kwa Tanzania Tech‘ jumuiya yenye lengo la kufanya au kutangaza kitendo kilicho kinyume cha sheria inapigwa marufuku vikali. • Unakubali kuwasilisha au kubadilishana na jumuiya za Tanzania Tech‘ michango ambayo ni kazi yako halisi tu. Usivunje, kunakili au kukiuka haki za Tanzania Tech au pande nyingine ikiwemo hakimiliki, alama za biashara, siri za kibiashra, faragha, kujitangaza, mtu binafsi au haki za wamiliki.

Iwapo Una Umri Chini ya Miaka 16:

• Tafadhali pata idhini ya mzazi au mlezi kabla hujashiriki katika jumuiya zozote zile za Tanzania Tech‘ .

• Kamwe usitoe maelezo binafsi kuhusu wewe mwenyewe au mtu mwingine yeyote yule (kwa mfano shule, namba ya simu, jina lako kamili, anwani ya nyumbani au anwani ya barua pepe).

Iwapo Utakiuka Kanuni Hizi za Jumuiya:

Iwapo utakaidi kufuata kanuni hizi za Jumuiya (na/au zinginezo tofauti katika shirika la eneo husika) wakati unashiriki katika Tanzania Tech‘ jumuiya, utatumiwa ujumbe wa barua pepe unaokufahamisha kwanini mchango wako umekataliwa au kuhaririwa. Ujumbe huu utajumuisha pia onyo kuwa kuendelea kukiuka kanuni hizi kunaweza kusababisha hatua kuchukuliwa dhidi ya akaunti yakoau zako.

Hatua hii huenda ikajumuisha mchango wowote uliotumwa na wewe kuangaliwa kabla ya kuruhusiwa kwenda katika tovuti au kusitishwa kwa muda au moja kwa moja uwezo wako wa kushiriki katika eneo au maeneo yoyote ya jumuiya za Tanzania Tech‘ .

Iwapo utawasilisha au kubadilishana mchango wenye kukera au usiokubalika kwa, au na jumuiya zozote zile za Tanzania Tech‘ au popote pale katika Tanzania Tech‘ au vinginevyo kujihusisha katika mwenendo wowote ule wa kuvuruga katika Tanzania Tech‘ , na Tanzania Tech inafikiria athari za mwenendo kama huo kuwa kubwa na/au kurudiwa tena,Tanzania Tech huenda ikatumia maelezo yoyote yale yanayopatikana kuzuia ukiukwaji zaidi kutokea. Hii inaweza kuwa ni pamoja na kuzifahamisha pande nyingine kama vile mwajiri, shule au mtoa huduma ya email kuhusu ukiukaji huo. Tanzania Tech ina haki ya kufuta mchango wowote ule,au kuchukua hatua dhidi ya akaunti yoyote ile ya Tanzania Tech, wakati wowote, kwa sababu yoyote ile.

Kukana na Kupunguza Wigo wa Uwajibikaji

15. Sehemu kubwa ya mchango unaotumwa katika jumuiya za Tanzania Tech‘ inafanywa na umma. Maoni yanayotolewa ni ya kwao na isipokuwa pale imeelezwa vinginevyo maoni hayo si ya Tanzania Tech au Tanzania Tech Media. Tanzania Tech na Tanzania Tech Media haihusiki na mchango wa maelezo yoyote yaliyotumwa na umma katika Tanzania Tech‘ au kwa upatikanaji wake au mchango wa tovuti za wa upande mwingine wowote ule zinazopatikana kupitia Tanzania Tech‘ . Viunganishi vyovyote vile kwa upande mwingine wa tovuti kutoka Tanzania Tech‘ haimaanishi tovuti hiyo imeidhinishwa na Tanzania Tech au Tanzania Tech Media na matumizi yoyote ya tovuti hiyo ni kwa athari yako mwenyewe.

16. Michango ya Tanzania Tech‘ , ikiwemo maelezo, majina, picha, logo, zinazohusiana na Tanzania Tech na Tanzania Tech Media, ni bidhaa na huduma (au kwa upande mwingine wa bidhaa na huduma), inatolewa “KAMA NI” na katika “KAMA INAVYOPATIKANA” kimsingi. Katika kiwango kinachoruhusiwa kisheria, Tanzania Tech inaondoa uwakilishi na udhamini wote (iwe imeelezewa au kumaanishwa kisheria), ikiwemo udhamini unaomaanishwa katika kiwango cha kuridhisha, kufaa kwa dhumuni maalum, isiyokiuka, inayokubaliana, ulinzi na usahihi. Tanzania Tech haihakikishii muda maalum, umalizikaji au utendendaji kazi wa tovuti au maelezo yoyote yale. Wakati tunajaribu kuhakikisha kuwa maelezo yote yanayotolewa na Tanzania Tech ni sahihi wakati wa uchapishaji, hakuna lawama yoyote inayopokelewa na au kwa niaba ya Tanzania Tech kwa makosa yoyote yale, kusahauliwa au maelezo yasiyo sahihi katika tovuti.

17.Hakuna kitu chochote katika masharti haya kinachoiondolea Tanzania Tech uwajibikaji au lawama juu ya kifo au maumivu yanayosababishwa na uzembe wake uliothibitibitika. Kwa mujibu wa sentensi iliyotangulia, Tanzania Tech na Tanzania Tech Media haitawajibika kwa upotevu wowote ule au uharibifu ufuatao (iwe uharibifu huo au upotevu ulitabirika, kujulikana au vinginevyo): (a) kupotea kwa data; (b) kupotea kwa mapato au faida iliyotarajiwa; (c) kupotea kwa biashara; (d) kupotea kwa nafasi; (e) kupotea kwa nia njema au kuathirika kwa hadhi; (f) upotevu ulizoziathiri pande nyingine; au (g) matokeo au athari yoyote ile isiyo ya moja kwa moja maalum au uharibifu unaotokana na matumizi ya Tanzania Tech‘ bila kujali kuchukuliwa hatua.

18.Tanzania Tech na Tanzania Tech Media haitoi hakikisho kuwa ufanyaji kazi unaopatikana katika Tanzania Tech‘ hautaingiliwa au kutokuwa na makosa, kwamba makosa yatarekebishwa, au kwamba Tanzania Tech‘ au seva inayowezesha upatikani wake haiwezi kuwa na virusi. Unakubali kuwa ni wajibu wako kutumia utaratibu unaohitajika na kukagua virusi (ikiwemo kipinga virusi na ukaguzi mwingine wa kiusalama) kutosheleza mahitaji yako maalum kwa usahihi wa data zinazoingia na kutoka.

20. Kushindwa au kuchelewa kwa Tanzania Tech kutekeleza au kusimamia yoyote kati ya masharti haya haiiondolei Tanzania Tech haki hiyo.

Wiji

Kwa kupakua na kusanikisha programu za Tanzania Tech zinazoweza kufutikwa (“Wiji ya Tanzania Tech”) na kutumia kuonyesha maudhui ya Tanzania Tech (“Maudhui ya Tanzania Tech”) kwenye kompyuta yako unakubaliana na masharti yaliyoainishwa hapo chini.

Masharti ya Wiji

3. Waranti & Uwajibikaji

3.1 Wiji za Tanzania Tech na Maudhui ya Tanzania Tech zinaundwa kwa msingi wa “kama zilivyo” na “kama zinavyopatikana” na unapakua, kusanikisha na kutumia Wiji za Tanzania Tech na kuangalia Maudhui ya Tanzania Tech kwa utashi na madhila yako.

3.2 Tanzania Tech imechukua tahadhari kuhakikisha kuwa Wiji za Tanzania Tech Widget na Maudhui ya Tanzania Tech kuepusha upungufu, makosa, virusi au hitilafu, hata hivyo Tanzania Tech haisemi kila kitu kitafanya kazi bila matatizo.

3.3 Kadri inavyoruhusiwa kisheria, Tanzania Tech haitoi hakikiso la aina yoyote (lidhaniwalo, lazima ay vinginevyo) kuhusiana na Wiji ya Tanzania Tech, Maudhui ya Tanzania Tech au tovuti ya Tanzania Tech na Tanzania Tech haitahusika kwa hasara yoyote au uharibifu utakaotokana au kuhusishwa na Wiji ya Tanzania Tech au Maudhui ya Tanzania Tech.

3.4 Unashauriwa kuchukua tahadhari zote kulinda kompyuta yako isiambukizwe virusi.

3.5 Tanzania Tech inaweza kubadilisha Maudhui ya Tanzania Tech kwa utashi wake na inaweza kuzuia matumizi ya Wiji ya Tanzania Tech endapo utakiuka Sheria hizi za Mtumizi wa Mwisho.

4. Jumla

Ujumla

* Iwapo masharti yoyote katika haya yanaonekana kuwa ni kinyume cha sheria, batili au vinginevyo hayawezekani kutekelezeka kutokana na sababu za kisheria katika nchi au jimbo lolote lile ambako masharti haya yamelengwa kufanya kazi, basi kwa kiwango na ndani ya uwezo wa kisheria ambako masharti hayo ni kinyume na sheria, batili au hayatekelezeki, yatafutwa kutoka katika masharti haya na masharti yaliyobaki yataendelea kuwepo na kutumika.

* Kushindwa au kuchelewa kwa Tanzania Tech kufanyia kazi au kutekeleza haki yoyote ile katika masharti haya haiondolei Tanzania Tech haki ya kutekeleza haki hiyo.

* Matumizi ya tovuti ya [Tanzania Tech‘ ] yanahusishwa na masharti na kanuni za Tanzania , ambayo ni lazima yatafsiriwe kulingana na sheria ya Tanzania na kuhusishwa chini ya uwezo wa kipekee wa kimahakama katika mahakama za Kitanzania.

Hitimisho

Iwapo una maswali maalum kuhusu Masharti ya Matumizi haya, tafadhali tuma ujumbe wa barua pepe email kupitia ukurasa wetu wa mawasiliano hapo chini.

Vigezo na mashari haya yame hakikiwa na tarehe 04/03/2021