in

Hatimaye Apple Yazindua Simu za iPhone 8 za Rangi Nyekundu

Hatimaye Apple imezindua simu hizo mpya za iPhone 8 RED

Hatimaye Apple Yazindua Simu za iPhone 8 za Rangi Nyekundu

Baada ya kupata habari kuhusu ujio wa simu mpya za iPhone 8 pamoja na iPhone 8 Plus za rangi nyekundu, hatimaye kampuni ya Apple imezindua simu hizo muda mchache uliopita. Simu hizo maalum kwa jina la iPhone 8 RED zimezinduliwa kwasababu ya ushirikiano wa kampuni ya Apple na shirika la RED ambalo kama nilivyo sema awali ni shirika la kusaidia waafrika kujilinda na UKIMWI (HIV/AIDS).

Sasa tukirudi kwenye simu hizo mpya, kama nilivyosema awali simu hizo hazina utofauti na simu za kawaida za iPhone 8 kwa upande wa sifa, bali zenyewe zinakuja na rangi nyekundu na bei yake inakuwa tofauti kidogo. Simu hizi kwa mwaka huu zinakuja na Rangi nyekundu kwa nyuma lakini kwa mbele zinakuja na rangi nyeusi. Kuhusu bei simu hizi zitanza kuuzwa kuanzia siku ya ijumaa ya mwezi huu April 13 lakini unaweza kuanza kutoa oda yako kuanzia kesho tarehe 10 April.

Bei ya simu hizi ya hizi kwa upande wa iPhone 8 RED ya kawaida yenye GB 64 itakuwa inauzwa dollar za marekani $699 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,600,000 na iPhone 8 RED Plus yenye GB 64 itakuwa inauzwa dollar za marekani $799 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,810,000. Kumbuka bei hizi zitaongezeka kwa Tanzania na viwango hivyo ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo.

Usinunue Simu ya Android au iPhone ya Zamani

Mbali na hayo Apple pia imezindua kava la rangi nyekundu ambalo litakuwa maalum kwa simu ya iPhone X au iPhone 10, kava hili ni yale ya kufunika kabisa kioo kama inavyo onekana hapo chini.

Kuhusu bei ya kava hilo jipya la iPhone X litakuja likiwa linauzwa dollar za marekani $99 sawa na Tsh 225,000. Kava hilo litaanza kupatikana sambamba na iPhone 8 RED yaani hapo siku ya kesho yaani tarehe 10 april lakini yatawafikia watumiaji tarehe 13 ya mwezi huu.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.