Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Habari Kubwa za Teknolojia kwa Wiki Hii (19/06/2016)

tech wiki tech wiki

Karibuni tena kwenye kipengele cha tech wiki hapa unapata kujua habari zote za teknolojia zilizovuma kwenye blog ya tanzania tech, pia tunaomba radhi kwa  kutokana na kutokwepo kwa kipengele hichi kwa siku zilizopita hii ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu ila kwa sasa kipengele hichi kita-kuwepo kila jumapili bila kukosa.

Samsung kwa mara nyingine tena ilizindua hizi earbuds zenye uwezo wa kupima moyo wako na hatua pale utakapo kua unatembea iki ni lengi la kuangalia afya yako.

Advertisement

Kampuni inayojulikana kama onvi imezindua msaki ambao unaweza kuangalia ndani ya mdomo wako pale unapokua unaswaki soma habari hii pamoja na video ya mswaki huo.

Hatimaye simu bomba ya huawei p9 imefika nchini south africa hii inawezekana kuwa simu hiyo ikaja tanzania pia na sehemu zingine za afrika mashariki soma habari hii upate kujua zaidi.

Tanzania imezidi kupiga hatua kuelekea kwenye ulimwengu mpya wa teknolojia, hivi karibuni airtel na veta tanzania wameungana na kuleta programu mpya ya veta somo inayokusaidia kupata masomo kupitia simu yako ya mkononi soma zaidi hapa.

Huduma za usafirishaji za Uber sasa zimefika nchini tanzania huduma hizo mpya zikiwa sasa zimesha fika afrika ma shariki sasa zimefika tanzania rasmi, kama unatafuta ajira kwenye sekta ya udereva soma hii.

Lenovo ya vunja kule kusubiri kwa kutengeneza simu yake ya kwanza yenye uwezo wa kujikunja simu hii ilizinduliwa kwenye tamasha la kampuni hiyo lililofanyika wiki iliyopita soma hii uone simu hizo live zikiwa zinafanya kazi.

Jifunze namna rahis ya ku-qute meseji kwenye programu ya whatsapp cheki na video ya hatua hizo moja kwa moja ili uweze kujifunza kwa urahisi zaidi.

Cheki hapa uzinduzi rasmi wa baadhi ya bidhaa za apple live kwenye mkutano wa Apple WWDC 2016 ambao ulifanyika huko marekani cheki video ya tukio zima hapa.

Soma hii ujifunze namna rahisi ya kutumia akaunti mbili za kila programu kwenye smartphone yako njia hii ni rahisi na salama kabisa soma hii ujifunze zaidi.

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka, pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa Tanzania tech blog. Pia usisahau kubofya hako ka-LOVE hapo chini ili ku-show love..!!

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use