in

Mtandao wa YouTube Wadukuliwa na Video Maarufu Kufutwa

Nyimbo maarufu zimefutwa na baadhi ya nyimbo kubadilishwa majina

Mtandao wa YouTube Wadukuliwa na Video Maarufu Kufutwa

Habari za hivi punde kutoka mtandao wa The Verge zinasema mtandao wa YouTube umedukuliwa na video maarufu kufutwa. Habari hizo zinasema kuwa video maarufu ambayo ndio ilikuwa maarufu kuliko zote ya Luis Fonsi na Daddy Yankee’s “Despacito, imefutwa kwenye mtandao huo na kava lake kubadilishwa na kuwekwa kava la watu wakiwa wameshika bunduki.

Pia baadhi ya nyimbo zenye view nyingi kama nyimbo za Chris Brown, Shakira, DJ Snake, Selena Gomez, Drake, Katy Perry, pamoja na Taylor Swift zimefutwa na  hazipo kabisa kwenye mtandao huo. Hata hivyo wadukuaji hao walijio jitambulisha kwa majina ya Prosox na Kuroi’sh, bado haijaulikana kama walidukua mtandao huo wa YouTube au akaunti binafsi za wasanii hao au akaunti za mtandao wa Vevo.

The Verge imewasiliana na mtandao wa Youtube kuhusu hilo na imeahidi kutoa taarifa zaidi kuhusu hilo. Hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza habari zaidi kuhusu udukuaji huu pale tutakapo zipata taarifa kutoka kwenye mtandao wa The Verge.

Updated Tarehe 4/10/2018 Saa 6:35PM – Baada ya the Verge kuwasiliana na YouTube, Youtube ilitoa maelezo kuwa udukuaji huo hausishwi na YouTube bali unahusisha Akaunti ya VEVO, na kwa mujibu wa msemaji wa VEVO, Tayari baadhi ya video zimesha fanikiwa kurudishwa na uchunguzi unaendelea kujua zaidi kuhusu Udukuaji huo.

Tigo Pesa Mastercard Kwa Manunuzi Mtandaoni

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.