in

Instagram Imeleta Sehemu ya Focus Kwenye iOS na Android

Baada ya majaribio sehemu hiyo sasa imekuja rasmi kwenye instagram

Instagram Imeleta Sehemu ya Focus Kwenye iOS na Android

Hivi karibuni Instagram imekuwa ikijikita zaidi kwenye maboresho ya sehemu yake ya Stories na baada ya majaribio ya muda mrefu hapo jana instagram imeanza kuleta sehemu mpya ya Focus kwenye App zake za Android na iOS.

Kama tulivyosema awali kwenye makala ya kuhusu ujio wa sehemu hii, sehemu hii inakusaidia kuweza kuchukua picha ya sura yako vizuri na huku kwa nyuma kukiwa hakuonekani vizuri, yaani kunakuwa na ukungu flani au kwa kitaalam (blur). Sasa sehemu hiyo mpya ya Focus kwenye Instagram itakusaidia kuweza kupiga picha za aina hiyo, ambazo zitakuwa zina angalia zaidi sura yako kuliko sehemu nyingine za mazingira ya mahali unapo piga picha.

Kama unavyo ona kwenye picha hapo juu sehemu hiyo ya Focus imeng’arisha zaidi sura za watu kuliko maeneo mengine kwenye picha hiyo. Sehemu hii mpya ya Focus imesha anza kupatikana rasmi na unaweza kuipata kwenye sehemu ya kamera kupitia programu yako ya Instagram, kumbuka hiyo ni mara baada ya ku-update programu hiyo.

Apps Nzuri za Kufuatilia kwa Karibu Kombe la Dunia

Hakikisha una angalia update za App ya Instagram kupitia soko lako la Play Store kama unatumia Android na App Store kama unatumia iOS ili kupata sehemu hiyo mpya.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments