Kampuni ya OpenAI hivi karibuni imetangaza kuja na jukwaa maalum ambalo litakuwa kwa ajili ya watafutaji wa ajira. Kwa mujibu wa muongozaji wa programu wa OpenAI, Fidji Simo amesema kupitia makala maalum kuwa mtandao huo utakuwa ukiitwa “OpenAI Jobs Platform”.
Matarajio ya mtandao huo yanategemewa kati kati ya mwaka 2026 huku ikitazamiwa kuwa mtandao huo utakuwa ni mshindani wa mtandao wa kijamii wa LinkedIn ambao unategemewa kwa sasa na watafutaji wengi wa ajira duniani.
Kwa mujibu wa Techcrunch, Kampuni ya OpenAI inatarajia kujikita kwenye bidhaa nyingine za kimtandao kama vile kuja na browser maalum inayotumia mfumo wa akili mnemba, pamoja na programu maalum ya mtandao wa kijamii.
Kwa sasa bado haijafahamika mtandao huo utafanya kazi vipi kwani unatazamiwa kuwa utakuwa mtandao shindani na Linkedin ambao unamilikiwa na kampuni ya Microsoft ambayo ni moja ya muwekezaji mkubwa wa kwenye kampuni ya OpenAI.