Simu za Infinix na TECNO Kupata Android 10 Kabla ya 2020

TECNO Spark 3 miongoni mwa simu zitakazopata Android 10
Simu za Infinix na TECNO Kupata Android 10 Kabla ya 2020 Simu za Infinix na TECNO Kupata Android 10 Kabla ya 2020

Kama wewe ni mmiliki wa simu ya TECNO au Infinix basi habari njema ikufikie kwani hivi karibuni kampuni hizo zinategemea kutoa mfumo mpya wa Android 10 kwa baadhi ya simu zake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Google, Transsion ambayo ni kampuni mama ya kampuni za Infinix, TECNO, pamoja na iTel imetangazwa kwenye list ya kampuni za simu ambazo zina tegemea kusasisha mfumo mpya wa Android 10 kwenye simu zake kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kampuni nyingine zilizotajwa kwenye list hiyo ni pamoja na ASUS, LG, Motorola, OPPO, Realme, Samsung, Sharp, Sony, na Vivo.

Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya XDA Developer, Google imetangaza kuwa kila simu ya Android ambayo inategemewa kuingia sokoni kuanzia mwaka 2020, ni lazima izinduliwe ikiwa na mfumo mpya wa Android 10 na sio vingine. Hii ni habari njema kwa watumiaji wa simu za TECNO na Infinix kwani kama unavyojua mara nyingi kampuni za TECNO pamoja na Infinix zimekuwa na utaratibu wa kuzinduwa simu mpya za Android zikiwa na mfumo wa zamani wa Android bila kujali kuwa kunao mfumo mpya wa Android kwa kipindi hicho.

Advertisement

Mbali na hayo, kampuni ya TECNO kwa sasa bado ipo kwenye majaribio ya mfumo huo wa Android 10 kwenye simu zake za Spark 3 Pro, ambapo simu hiyo inategemewa kuwa moja kati ya simu kutoka kampuni ya TECNO zitakazo pata mfumo huo mpya wa Android 10.

Simu za Infinix na TECNO Kupata Android 10 Kabla ya 2020

Mpaka sasa kampuni zote za TECNO na Infinix bado hazijatangaza list kamili ya simu ambazo zitapokea mfumo huo mpya wa Android 10 kabla ya mwisho wa mwaka huu 2019. Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, simu zote za TECNO Spark 3 Pro, TECNO Phantom 9, TECNO Camon 12, TECNO Spark 4, Infinix Hot 8 na Infinix S5 zinategemewa kuwa kwenye list ya simu zitakazo pata mfumo huo mpya.

Kwa sasa kama unamiliki simu ya TECNO Spark 3 Pro na unataka kujaribu mfumo huo wa Android 10 kwenye simu yako, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kwani tutakuletea hatua kwa hatua jinsi ya kuinstall mfumo huo kwenye simu yako. Kupata list nzima ya simu za TECNO na Infinix ambazo zitapata mfumo huo hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku au pakua app yetu kupitia soko la Play Store.

3 comments
  1. Kuna taarifa nmezisoma kwenye ukrasa wa Tecno Instagram kuhusu wateja wa Tecno wanaomiliki matoleo ya Camon kubadilisha simu zao kwa tsha 203000 nakupata toleo jipya la Camon 12,je habari hizi ni za kweli?

  2. Naomba msaada, natumia TECNO SPARK3 PRO nataka kui-root. Nisaidieni hapa nafanyaje niweze kufanikisha??

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use