Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Twitter Kufuta Akaunti Ambazo Hazijatumika kwa Miezi Sita

Kama akaunti yako haijatumika kwa miezi sita au zaidi basi ni wakati wa kutumia sasa
Twitter Kufuta Akaunti Ambazo Hazijatumika kwa Miezi Sita Twitter Kufuta Akaunti Ambazo Hazijatumika kwa Miezi Sita

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanamiliki akaunti kupitia mtandao wa Twitter na hujatumia akaunti yako kwa muda zaidi ya miezi sita basi habari hii ikufikie. Kwa mujibu wa msemaji wa Twitter, hivi karibuni twitter inategemea kuanza zoezi la kufuta akaunti ambazo hazijatumika kwa muda zaidi ya miezi sita.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, zoezi hilo linategemea kuanza kwa mtumiaji wa twitter kuokea email ambayo inakutaka kuingia kwenye akaunti yako kabla ya tarehe 11 ya mwezi wa 12 mwaka huu 2019. Hata hivyo baada ya kupokea email hiyo na endapo mtumiaji hatoingia kwenye akaunti yake, basi akaunti hiyo itafutwa na username kuachiwa kwajili ya kutumiwa na watu wengine.

Advertisement

Twitter Kufuta Akaunti Ambazo Hazijatumika kwa Miezi Sita

Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji huyo, akaunti hizo hazito futwa zote kwa pamoja bali itakuwa inatofautiana kwa kila mtumiaji, vilevile akaunti hizo zitafungwa miezi michache baada ya kupokea email au barua pepe yenye kutoa tahadhari juu ya kufutwa kwa akaunti yako.

Kwa sasa kama unataka kuepukana na tatizo hili, unaweza kutumia njia yetu ya jinsi ya kushare picha kutoka instagram kwenda Twitter. Njia hii ni nzuri kwa sababu kila ambacho utakuwa unapost kwenye akaunti yako ya Instagram basi moja kwa moja kitu hicho kitaenda kwenye akaunti yako ya Instagram bila wewe kufanya kitu chochote cha zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use