in

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5

Simu hii inakuja na kamera nne na mtindo mpya wa kioo chenye kitobo

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5

Hatimaye hivi leo oktoba 15, 2019 kampuni ya Infinix imezindua simu mpya ya Infinix S5 huko nchini India. Infinix S5 ni mrithi wa simu ya Infinix S4 ambayo ilizinduliwa hapa Tanzania takribani miezi mitano iliyopita.

Infinix S5 inakuja na muundo mpya kabisa wa kioo huku ikiwa na sehemu ya kamera ya mbele iliyopo ndani ya kioo au (Punch hole display), kioo hicho kime tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD huku kikiwa na urefu wa jumla ya inch 6.6 pamoja na resolution ya hadi pixel 720 x 1520.

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5

Simu hii inakuja na kamera za nne za nyuma, kamera kuu inakuja na 16-megapixel, nyingine zina kuja na megapixel 5 ambayo ni ultrawide, megapixel 2 ambayo ni depth sensor na megapixel 2 nyingine ambayo ni low-light. Kamera zote zina kuchukua video hadi [email protected]. Kwa upande wa sifa za kamera ya mbele Infinix S5 haina tofauti na Infinix S4 kwani nayo inakuja na kamera ya selfie ya yenye megapixel 32.

Kampuni ya Airtel ya Kwanza Kuja na eSIM Tanzania

Kampuni ya Infinix Yazindua Simu Mpya ya Infinix S5

Simu inakuja na chipset ya MediaTek MT6761 Helio P22 na nguvu ya CPU ya Octa-core (4×2.0 GHz Cortex-A53 na 4×1.5 GHz Cortex-A53). CPU hiyo inasaidiwa na RAM ya hadi GB 4 na uhifadhi wa ndani wa hadi 64 GB. Hifadhi ya hiyo ya ndani inaweza kuongezwa na memory card ya hadi GB 256. Sifa nyingine za Infinix S5 ni kama zifuatazo.

Sifa za Infinix S5

Soma hapa Sifa kamili za simu hii

Bei ya Infinix S5

Kwa upande wa bei Infinix S5 inatarajiwa kuingia sokoni nchini India hivi karibuni na inasemekana kuuzwa kwa rupee ya india ₹10,999 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Kitanzania TZS 354,000 bila kodi. Simu hii ina tegemewa kuuzwa kwenye soko la flipkart kwa bei ya punguzo.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

12 Comments