Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 4 Air

Simu hizi zinakuja na maboresho machache kutoka simu za Spark 3
Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 4 Air Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 4 Air

Kampuni ya TECNO hapo jana imezindua simu zake mpya za Spark 4 huko nchini India, simu ambazo ni muendelezo wa matoleo ya simu za Spark ambazo huzinduliwa mara moja kila mwaka.

Kwa mwaka huu kampuni hiyo imezindua matolea matatu, Tecno Spark 4, Spark 4 Air, pamoja na Spark Go. Simu hizi zote zinakuja na muonekano unaofanana kwa kiasi kikubwa lakini zote zinakuja na sifa tofauti kidogo.

Advertisement

TECNO Spark 4

Tukianza na Spark 4, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.52, kioo kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD chenye uwezo wa resolution hadi pixel 720 x 1600. Kioo hicho kinakuja na ulinzi maalum wa kuweza kuzuia kioo cha simu hiyo kuto kupata michubuko kwa urahisi.

Mbali na hayo Spark 4 inakuja na kamera moja ya selfie kwa mbele yenye uwezo wa Megapixel 8 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 720p@30fps. Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera tatu, huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 13 na nyingine mbili zikiwa na megapixel 2 na megapixel 0.3. Kamera zote tatu kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video hadi 1080p@30fps.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 4 Air

Spark 4 inaendeshwa na processor ya Mediatek MT6761 Helio A22 ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 4 na GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 32 na GB 64. Hata hivyo ukubwa huo unaweza kuongezwa na memory card ya hadi GB 128. Sifa nyingine za TECNo Spark 4 ni kama zifuatavyo.

Sifa za Tecno Spark 4

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.52 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1600 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core CPU (4×2.0 GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek MT6761
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na GB 32 na nyingine ikiwa na GB 64 zote ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili moja ina RAM ya GB 3 na nyingine ina GB 4
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.8, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.2 na kamera ya mwisho ni low light yenye Megapixel 0.3. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-ion 4000 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Royal Purple na Vacation Blue.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

TECNO Spark 4 Air

Kwa upande wa Spark 4 Air, simu hii inakuja na kioo ambacho ni kidogo kwa Spark 4. Simu hii inakuja na kioo cha inch 6.1 ambacho pia kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, kioo hicho kinakuja na resolution ya pixel 720 x 1560.

Tofauti na kioo, utofauti mwingine ulipo kati ya simu hizi pili ni pamoja na kamera. Spark 4 Air inakuja na kamera mbili ambazo zinauwezo wa Megapixel 13 pamoja na Megapixel 5 kamera zote zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 720p@30fps. Utofauti mwingine ni kamera ya mbele ambayo inakuja na Megapixel 5 ikiwa pia na uwezo wa kuchukua video hadi 720p@30fps.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 4 Air

Spark 4 Air inaendeshwa na processor ya Mediatek MT6761 Helio A22 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 3 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 32. Ukubwa huo unaweza kuongezwa na memory card ya hadi GB 128. Sifa nyingine za TECNo Spark 4 Air ni kama zifuatavyo.

Sifa za TECNO Spark 4 Air

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.1 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1600 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Quad-core CPU (4×2.0 GHz Cortex-A53).
  • Aina ya Processor (Chipset) – MediaTek MT6761
  • Uwezo wa GPU – PowerVR GE8320.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 32 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 128.
  • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 3
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 5.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/1.8, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.2. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya Dual LED Flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-ion 3000 mAh.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Royal Purple na Vacation Blue.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 4 Air

Kwa upande wa bei Tecno Spark 4 inatarajiwa kuzinduliwa hapa Tanzania mwezi ujao wa tisa na inategemewa simu hiyo itakuwa inauzwa kati ya Shilingi za kitanzania TZS 300,000 hadi TZS 280,000 pamoja na kodi. Spark 4 Air yenyewe inatarajiwa kuuzwa kwa kati ya TZS 240,000 hadi TZS 220,000 pamoja na kodi kumbuka bei hizi zinaweza kushuka au kupanda.

Kama unataka kujua sifa pamoja na bei ya Spark Go unaweza kutembelea ukurasa huu hapa.

8 comments
  1. Kwaufupi tecno ni simu nzur sana hasa katka suala la chaji iko vzr piah ni simu imara ila piah naomba kujua bei ya hii sim spark 4 kwasababu naitaji nitafute kwa watu tuliopo mikoani kama iringa bei yake ni shingapi!!!!!????????¿?? Ahsante

    Pia kwa uoande wa internal memory nikweli kwamba spark 3 ina ukubwa wa 32-64 GB?! Spark 4 namanisha sio 3

  2. Jamani mimi naitwa Denis nimenunua spark 4 sealed lakin RAM mbona iko na 2 na sio 3 je inamaana niliibiwa?????

    Jambo lingine niwaponfeze tuu Tecno kwa uzalishaji wa bidhaa bora na kwa bei ya kawaida.
    Ila naombeni ufafanuzi juu ya RAM.

  3. Nahitaji simu Tecno 4 Niko singida mjini
    Mimi ni mwenyekiti wa chama kikuu Cha ushirika mkoa wa singida
    Nimesoma maelezo kwa kiasi nimeridhika na tecno 4

  4. Nahtaj jua…mbona spark4 air Ina ram2…na kmaelezo mmesema ram3 betri isiyotokaaa ..mbona yangu yatokaaa….NISAIDIWEEE KIMAELEZOO

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use