Mabadiliko Mapya kwenye Mtandao wa YouTube (Muhimu Sana)

Mabadiliko haya yanahusu mtu yoyote mwenye channel YouTube
Mabadiliko Mapya kwenye Mtandao wa YouTube (Muhimu Sana) Mabadiliko Mapya kwenye Mtandao wa YouTube (Muhimu Sana)

Kama wewe ni mmoja wa watu wenye channel kupitia mtandao wa YouTube basi makala hii ni muhimu sana kwako. Kupitia makala hii nitakupa taarifa fupi yenye maelezo ya muhimu hasa kama unataka kuendelea kutumia mtandao wa YouTube ikiwa pamoja na kutengeneza pesa kupitia video hizo.

Sheria ya COPPA

Kupitia makala hii utakuwa ukiona neno moja linalo jirudia mara kwa mara, neno hilo ni COPPA. Kwa kirefu COPPA ni Children’s Online Privacy Protection Act, hii ni sheria ya marekani iliyotungwa mwaka 1998 ambayo nia yake ni kudhibiti ukusanyaji wa data unaofanywa na makampuni ya marekani kwa watoto chini ya umri wa miaka 13.

Sheria hii inafanya kazi kwa kampuni zote zenye makao yake makuu nchini marekani hata kama kampuni hizo zinafanya kazi nje ya Marekani. Hii ni sawa na kusema, sheria hii ya COPPA inafanya kazi kwenye biashara zote za kampuni yoyote ya ambayo ina makao yake makuu nchini marekani bila kujali kwamba kuna sheria nyingine kwenye nchi husika.

Advertisement

Kwa upande wa YouTube, sheria hii ilianza kufanyiwa kazi kwa muda mrefu kidogo ikiwa pamoja na kuandaa mifumo ambayo itasaidia watumiaji wa mtandao huo kutii vigezo na masharti ya sheria hiyo ya COPPA. Kumbuka ni lazima watumiaji wote wa YouTube kutii vigezo na Masharti hayo bila kujali unatokea nchi gani ili mradi tuu.. unatumia mtandao wa YouTube kusambaza video zako.

Mabadiliko ya YouTube

Sasa hivi karibuni YouTube imefanya mabadiliko kwa watumiaji wote wa mtandao wake, mabadiliko hayo yanawataka watu wote wanaotumia matandao huo kusambaza video zao kutii vigezo na masharti ya Sheria ya COPPA hasa kama unayo channel yenye kulenga zaidi watoto chini ya umri wa miaka 13. Mbali na hayo channel zote zinatakiwa kuonyesha maudhui yake ni kwa ajili ya watu gani (Watoto chini ya miaka 13 au Watu wazima) kwenye kila video inayo wekwa kwenye mtandao huo ikiwa pamoja na kwenye kila channel husika.

Kama wewe ni mmoja wa watu wenye channel kupitia YouTube unatakiwa kuonyesha kama channel yako inalenga watoto chini ya umri wa miaka 13 au inalenga watu wazima, ni muhimu kufanya hivyo kwani kwa kukiuka vigezo na masharti hayo channel yako inaweza kuwekwa na YouTube kama ni channel ya watoto au channel ya watoto inaweza kuwekwa kama channel ya watu wazima na kuna hasara inayotokana na YouTube kufanya hivyo badala yako.

Jinsi ya Kutii Vigezo na Masharti ya COPPA

Baada ya kipindi chote cha kujiandaa kutii sheria ya COPPA, hatimaye sasa YouTube imeleta sehemu mpya ambazo zitakusaidia wewe kutii Masharti ya sheria hiyo kwenye channel yako. Ili kutii vigezo hivyo unatakiwa kuonyesha kama channel yako inalenga watoto au watu wazima na unaweza kufanya hivyo kupitia sehemu ya Settings > Channel > Advanced Settings > Audience kisha china yake utaona sehemu mbili moja yenye sentensi inayoanza na Yes, na nyingine inayo anza na No,.. Kama channel yako inalenga zaidi watoto unatakiwa kuchagua Yes, kama hailengi kabisa watoto changua No.

Mabadiliko Mapya kwenye Mtandao wa YouTube (Muhimu Sana)

Kwa kufanya hivyo video zako zote zitakuwa zimewekwa kwa ajili ya watoto kama umechagua Yes na kwa ajili ya watu wazima kama umechagua No. Kama kwa namna yoyote channel yako inayo mchanganyiko wa video za watoto na za watu wazima basi ni vyema kutumia njia ya kutii vigezo hivyo kupitia kwenye kila video. Unaweza kufanya hivyo kwa kufuata hatua hizi, ingia kwenye Video Manager > Videos kisha chagua video unazodhani ni kwa ajili ya watoto kisha bofya Edit alafu chagua Audience na na chagua Yes kwama video hizo ni kwa ajili ya Watoto.

Mabadiliko Mapya kwenye Mtandao wa YouTube (Muhimu Sana)

Mbali na hayo, pia kila mara utakapokuwa una weka video mpya kwenye mtandao wa YouTube utaulizwa kama video hiyo ni kwa ajili ya watoto au watu wazima hivyo utaweza kubadilisha kwa haraka kwenye kila video unayoweka kwenye mtandao huo.

Mabadiliko Mapya kwenye Mtandao wa YouTube (Muhimu Sana)

Mabadiliko kwa Channel Kwaajili ya Watoto

Sasa kutokana na mabadiliko hayo YouTube imeanisha baadhi ya vitu ambavyo unatakiwa kuangalia ili kuchagua sehemu ya kukubali kama channel yako ni kwaajili ya watoto, vigezo hivyo ni pamoja na

  • Mada ya Video yako au channel yako inahusu watoto
  • Kama Kuna watoto kwenye video yako
  • Kwenye video yako kuna vitu kwaajili ya watoto kama vile, nyimbo za kitoto, katuni au midoli kwaajili ya watoto n.k
  • Kwenye video yako unatumia lugha ya kitoto au lugha ambayo inatumiwa na watoto
  • Kuna vitu (picha, sauti, n.k) ambavyo vinafaa kwa watoto
  • Kuna hadithi, nyimbo au mashairi kwaajili ya watoto.

Kama video yako au channel yako inayo vitu hivyo basi ni lazima kuhakikisha unachagua sehemu ya kuwa channel yako ni kwaajili ya watoto. Kumbuka vitu hivyo ni baadhi tu ya vitu ambavyo vinaweza kufanya channel yako iwe ni kwaajili ya watoto. Kitu cha muhimu ni kuangalia wewe mwenyewe na kuhakikisha unachagua sehemu ambayo ni sahihi. Unaweza kusoma zaidi hapa.

Je Inakuwaje Kama Channel Yako ni Kwaajili ya Watoto

Mbali ya yote hayo hapo juu yapo mabadiko ambayo yatakuwepo kwenye channel ambazo zitachagua au zimechaguliwa kuwa na maudhui kwaajili ya watoto. Mabadiliko hayo ni pamoja na

  • Kwenye Video au channel za watoto kutakuwa hakuna sehemu ya Comment (Maoni)
  • Kwenye Video au channel za watoto kutakuwa hakuna matangazo mengi au matangazo yanayolenga sehemu au aina ya kitu unachofanya mtandaoni. Hii inaweza kufanya channel au video kwaajili ya watoto kuingiza pesa kidogo kutokana na matangazo.
  • Pia sehemu kama Info Card, Notification, End Screen, Watch Later, na Save to Playlist zote zita ondolewa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka 2020.

Hayo tu ni baadhi ya mambo ambayo yatabadilika kwa channel ambazo ni kwaajili ya watoto, pia YouTube imeainisha kuwa mabadiliko mengine yanaweza kutoka kwani bado wanaendelea kufanya majaribio ya sehemu mbalimbali ili kukidhi vigezo na masharti ya sheria hiyo ya COPPA. Kama unataka maelezo zaidi unaweza kuangalia video hapo chini.

Mpaka hapo natumaini umeweza kuelewa kikamilifu, kama unayo channel kwenye mtandao wa YouTube ni muhimu kuhakikisha unafuata vigezo na masharti hayo kwani hii inawez kusabaisha channel yako kupoteza mapato au kupata adhabu ambazo YouTube hawaja zitaja. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma vigezo na masharti ya YouTube kwa kiswahili kupitia hapa. Kujua kuhusu mabadiliko mengine ya YouTube yaliyopita soma hapa.

Kuwa wa kwanza kupata habari kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku, pia usisahau kupakua toleo jipya la app ya Tanzania Tech kupitia Play Store. K

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use