Jinsi ya Kuangalia Movie Netflix Bure Bila Kulipia (Bila Akaunti)

Utaweza kuangalia movie mpya za Sasa kutoka Netflix bila kulipia
Jinsi ya Kuangalia Movie Netflix Bure Bila Kulipia (Bila Akaunti) Jinsi ya Kuangalia Movie Netflix Bure Bila Kulipia (Bila Akaunti)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao ni wapenzi wa Movie basi ni wazi kuwa ulishawahi kutafuta njia za kuweza kuangalia movie za Netflix Bure bila mafanikio. Japo kuwa hakuna njia ya moja kwa moja ya kuangalia movie kutoka Netflix bure, lakini zipo njia kadhaa ambazo zinaweza kukusaidia kupata Movie za Netflix na kuangalia bure.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia moja ambayo unaweza kutumia kuweza kuangalia movie hizo za Netflix bure na bila kuangaika kutengeneza akaunti, basi bila kuendelea kuandika maneno mengi moja kwa moja twende kwenye njia hii rahisi.

Kwa kuanza unatakiwa kuwa na simu ya Android, kama tayari unayo simu ya android moja kwa moja unaweza kupakua app kupitia link hapo chini.

Advertisement

Download App Android Hapa

Pia app hii inapatikana kwa watumiaji wa Windows na Mac na unweza kupakua kulingana na mfumo wako kwa kuchagua link husika.

Download App Windows

Kupitia app hii, setup zote zinafanana hivyo haijalishi unatumia Android au Windows utaweza kufanya setup hizi kwa kufuata hatua hizi hapo chini.

Baada ya kupakua na kuinstall app hii kwenye simu yako moja kwa moja sasa endelea kwenye hatua hizi. Hatua ya kwanza bofya kitufe cha jumlisha kilichopo juu upande wa kulia.

Jinsi ya Kuangalia Movie Netflix Bure Bila Kulipia (Bila Akaunti)

Baada ya kubofya hapo saa utapata nafasi ya kuweza kuandika link, kwenye sehemu hiyo ya kuandika link andika maneno haya huhu.to hakikisha unaandika kama ilivyo bila kuacha nafasi na kuweka hakikisha unaweka dot kabla ya neno to kama invyo onekana kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kuangalia Movie Netflix Bure Bila Kulipia (Bila Akaunti)

Baada ya hapo bofya Continue kisha subiri kidogo na moja kwa moja utaweza kuona list ya movie za Netflix na utakuwa upo tayari kuangalia movie yoyote ya Netflix bure na bila kuwa na akaunti.

Jinsi ya Kuangalia Movie Netflix Bure Bila Kulipia (Bila Akaunti)

Kuangalia movie yoyote bofya movie yenyewe kisha bofya kwenye sehemu ya Server chini ya maelezo ya movie na moja kwa moja utaweza kuona movie ikicheza kupitia kwenye simu yako. Hadi hapo natumaini umeweza kuangalia movie za Neflix bure, kama una maswali au maoni unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Kama unataka kujua app za kudownload movie kupitia simu yako ya mkononi basi unaweza kusoma hapa ili kudownload app hizo moja kwa moja. Kama unatafuta movie nzuri za kuangalia unaweza kuangalia list yetu ya Sunday Movie hapa.

3 comments
  1. nilikuwa naomba kuuliza apo unapokuwa umefanikiwa kuanza kutizama netflix bure unaweza ukazima data ya simu au nayo inatumika kama ilivyo kweny you tube vile ama?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use