Jinsi ya Kupata Namba ya Simu ya Nje ya Nchi Bure

Tumia njia hii kuweza kupata namba yako ya simu ya nje ya nchi
Jinsi ya Kupata Namba ya Simu ya Nje ya Nchi Bure Jinsi ya Kupata Namba ya Simu ya Nje ya Nchi Bure

Inawezekana kwa namna yoyote ukawa na uhitaji wa kupigiwa simu na watu kutoka nje ya nchi na uhitaji kutumia mitandao kama WhatsApp na mitandao mingine.

Kupitia maujanja haya leo nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kupata namba yako ya simu ya nje ya nchi na unaweza kutumia kupiga na kupigiwa simu bure kabisa, pia unaweza kutumia namba hiyo kusajili mitandao ya kijamii kama WhatsApp na mitandao mingine.

Kwa kuanza unahitaji vitu kadhaa, kitu cha kwanza cha muhimu ni Internet, unahitaji angalau kiasi cha MB 200 na kuendelea, pia unatakiwa kuwa na akaunti ya Facebook au Google. Kama tayari unavyo vitu vyote hivi basi unaweza kuendelea hatua inayofuata.

Advertisement

Hatua ya kwanza Download app hapo chini kisha install kwenye simu yako, kwa sasa app hii haipo kwa Tanzania hivyo hakikisha unapakua app hii kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii, subiri kwanza na Husijisajili kupitia app hiyo, unacho takiwa kufanya moja kwa moja bofya hapo chini na utapelekwa kwenye tovuti rasmi ya App hiyo, kisha tengeneza akaunti yako kwa kutumia akaunti yako ya Google, baada ya hapo sasa unaweza ku-login kwa kutumia akaunti yako yako kupitia app uliyo download moja kwa moja.

Tembela Tovuti Hapa

Baada ya hapo unaweza kuangalia video hapo chini kujua jinsi ya kutumia app hii na kupata namba yako ya simu ya nje ya nchi moja kwa moja kupitia simu yako ya Android.

Njia hii itakusaidia sana kupiga simu za nje ya nchi na pia utaweza kupata namba ya simu ambayo utaweza kutumia kupiga simu kwa urahisi na haraka, pia unaweza kupigiwa ndani ya namba yako moja kwa moja.

Kitu cha msingi hakikisha namba yako unaitumia kwani usipo itumia kwa muda mrefu namba hiyo inaweza kufutwa na kupewa mtu mwingine au inaweza kufutwa kabisa na hutoweza kuipata.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujia jinsi ya kuona namba ya simu ya mtu yoyote ambaye unachati nae kwenye mtandao wa Facebook.

15 comments
  1. Maoni*nmekipenda sana elimu yenu …lakini naomba pia kupata elimu ya jinsi ya kuhack chat za mtu mwingine za watsup ambaye ako mbali na mimi .shkuraniii nyotee

  2. Nimesha download app hiyo Yalp lkn bado nikijaribu kuidownload text now inagoma na hapo nimeweka kuipata kupitia Yalp bado inagoma

  3. Jaman nipo omani nataka niwe natumia line yangu ya Tanzania kuunganishwa MB nifanyaje hadi mtu wa tanzania awe ananiunganisha na Mb za hk

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use