Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Instagram Yazindua App Mpya ya Instagram Lite (Download)

Programu ya Instagram Lite yazinduliwa Kimya kimya
Instagram Lite App Instagram Lite App

Hivi karibuni mtandao wa instagram umetangaza kwa sasa umefikisha watumiaji zaidi ya Bilioni 1, wakati watumiaji hao wakizidi kuongezeka kila siku, hivi karibuni instagram imezindua app ya Instagram Lite kwaajili ya simu zenye uwezo mdogo.

Kama unavyojua watumiaji wengi zaidi wa mtandao wa instagram ni wale wenye simu zenye uwezo mkubwa kidogo, kwani programu ya Instagram inakuja ikiwa na ukubwa wa MB 100 au zaidi kulingana na kifaa au simu yako.

Advertisement

Kuliona hilo na kuhakikisha Instagram inawafikiwa watu wengi zaidi, sasa imeleta app ya mpya ya Instagram Lite ambayo inakuja na ukubwa wa MB 1 tu. Kama zilivyo programu nyingine za Lite, Instagram Lite ni kwaajili ya simu zenye ukubwa mdogo wa ndani (Internal Memory) pamoja na wale wenye simu zenye uwezo mdogo. Hata hivyo unaweza kutumia programu ya Lite kwenye simu yoyote, lakini kwa sasa programu hiyo imezinduliwa nchini Mexico pekee na itakuja kwa watumiaji wengine baadae mwaka huu kupitia masoko ya App Store na Play Store.

Lakini kama unataka kujaribu programu hiyo ya Instagram Lite sasa hivi, unaweza kufanya hivyo kwa kupakua app hiyo kwa kupitia LINK HAPA.

Utofauti pekee uliopo kwenye app hii ya Instagram Lite na App ya kawada ya Instagram, kupitia App hiyo utoweza kuona video za IGTV na pia hutoweza kupakia video kupitia app hiyo. Mbali na hayo sehemu nyingine zinafanya kazi kama ilivyo kwenye app ya kawaida ya Instagram.

Kama umefanikiwa kupakua app hii mpya ya Instagram, tuambie kwenye maoni hapo chini unaonaje App hiyo. Kwa watumiaji wa iOS bado hakuna taarifa za ujio wa App hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use