Apps #18 App Nzuri za Kudownload Filamu Kwenye Simu

Kama wewe ni mpenzi wa filamu (Movies) unasoma makala sahihi
App nzuri za kudownload Movies App nzuri za kudownload Movies

Habari ya jumapili na karibu kwenye makala nyingine ya App nzuri, siku ya leo nimekuletea app nzuri za kuweza kusaidia kudownload filamu kupitia simu yako ya mkononi ya mfumo wa Android. App hizi nilizokuandalia siku ya leo hazipatikani kupitia soko la Play Store hivyo, nimekuandalia link maalum ambazo utatumia kuweza kupakua app hizi moja kwa moja kupita simu yako ya Android.

Nachokuahidi kwenye sehemu hii ya 18 ya App nzuri ni kuwa, App hizi zitakupa urahisi sana wa kupata filamu yoyote, tamthilia (series) mbalimbali pamoja na kuwa na uwezo wa kuangalia trailer au hata filamu hizo moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi. Najua leo ndio siku yako ya kupumzika basi bila kupoteza muda twende tukangalie app hizi nzuri.

1. TeaTV

TeaTV ni app ya kwanza kwenye list hii app hii intakupa uwezo wa kupakua filamu, series na hata tamthilia kwa haraka sana. App hii ni rahisi sana kutumia na inapatikana bure kabisa. Unaweza kupakua app hii kwa kubofya link hapo chini.

Advertisement

DOWNLOAD TEA TV

2. The Movie DB

The Movie DB ni appa nyingine nzuri sana ya kudownload movie na series, application hii itakupa uwezo wa kuchagua kulingana na mwaka, genre na pia tofauti na app iliyopita, App The Movie DB inayo sehemu ya filamu za katuni hivyo utaweza kudownload filamu za katuni (Animation) kwaajili ya yako au hata watoto wako. Kama kawaida link ya kupakua App hii iko hapo chini.

DOWNLOAD THE MOVIE DB

3. Show Box

Show Box ni Application nyingine bora kabisa kwaajili ya kudownload filamu, Application hii itakupa uwezo wa kupakua filamu, na tamthilia moja kwa moja kupitia sim yako ya Android. Kingine kiziri kuhusu App hii ni kuwa itakupa uwezo wa kusoma habari mbalimbali zinazohusiana na filamu mpya na hata zile zinazokuja huku ikikonyesha na Trailer za filamu hizo.

DOWNLOAD SHOW BOX

4. Popcorn Time

Popcorn time ni app nyingine nzuri sana kwaajili ya kupakua filamu, kupitia App hii utaweza kupata movie mpya kulingana na umaarufu wake. Mbali na movie pia utaweza kudownload series pamoja na animation moja kwa moja kupitia simu yako ya Android.

DOWNLOAD POPCORN TIME

5. Terrarium TV

Terrarium tv ni app nyingine nzuri sana kwaajili ya kupakua filamu, app hii nimekuwa nikitumia kwa muda mrefu sasa na kweli imekuwa ikinisaidia sana kupata filamu kwa wakati. App hii inakupa filamu na tamthilia mpya na uzuri ni kuwa kila filamu mpya itakapo kuwa inapatikana kupitia App hiyo basi utatumiwa ujumbe moja kwa moja ili uweze kupakua. Muhimu ni kuwa kumbuka kufuata hatua za muhimu ambazo tulionyesha kwenye makala iliyopita ili kupata filamu yenye muonekano mzuri, unaweza kuangalia video hapo chini kujua jinsi ya kutumia.

DOWNLOAD TERRARIUM TV

  • Jinsi ya kutumia App ya¬†Terrarium TV

LINK ZA APP KWENYE VIDEO HIZI HAPA

Na hizo ndio app nzuri nilizo kuandalia siku ya leo, Kama ulipitwa na sehemu ya 17 ya App nzuri unaweza kusoma makala hiyo hapa na uhakikia utapata app nzuri sana za kuweza kukusaidia kurahisha matumizi ya simu yako ya mkononi. Basi hakikisha unaendelea kutembelea Tovuti ya Tanzania Tech na pia usisahau kupakua app ya Tanzania Tech ili kupata habari kwa haraka zaidi.

Pia kama unataka kupata App za kuweza kukusaidia kudownload nyimbo mpya, unaweza kuzipata kwa kusoma makala yetu inayo onyesha jinsi ya kudownload nyimbo mpya kwa kutumia simu yako ya Android.

Makala imeongezwa Tarehe 10-11-2018 : Makala hii imeongezwa kwa kuweka maelezo ya jinsi ya kupata nyimbo mpya kwa kutumia simu yako ya Android.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use