Sasa Tumia Njia Mpya ya Kuuliza Maswali Kupitia Instagram

Sasa unaweza kuuliza maswali kwa maandishi kupitia instagram
Sehemu mpya ya Maswali Instagram Sehemu mpya ya Maswali Instagram

Hivi karibu Instagram ilikuwa ikifanya majaribio ya sehemu mpya ya kuuliza maswali kupitia sehemu ya Stories sasa majaribio hayo yamekiswa na sasa tayari sehemu hiyo inapatikana kwenye programu za Instagram za iOS na Android.

Sehemu hii mpya itakupa uwezo wa kuuliza maswali kwa maandishi tofauti ya sehemu ya Poll ambayo inakupa uwezo wa kuchagua peke yake. Sehemu hiyo mpya inakupa uwezo wa kuandika swali lako kupitia sehemu hiyo ya Stories na wafuasi wako wataweza kutoa majibu yako kwa kuandika jibu kupitia sehemu iliyoko wazi chini ya sehemu hiyo mpya.

Sehemu hii mpya inapatikana kupitia sehemu ya stika kisha utachagua stika iliyoandikwa Question na hapo utaweza kuandika swali lako kwa juu ya stika kisha malizia kwa kubofya Done na swali lako litakuwa linatokea kwenye sehemu ya Stories.

Advertisement

Kusoma majibu, majibu ya swali lako yatakuwa yanatokea kwa chini ya picha pamoja na idadi ya watu walio angalia picha hiyo pamoja na majina yao.

Sehemu hii kwa sasa tayari inapatikana kwenye programu zote za instagram za android pamoja na ios, kama bado hujapata sehemu hii akikisha una update programu yako ya instagram ya android au iOS.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use