Apps #17 App Mpya za Kujaribu Kwenye Simu ya Android

Application nzuri za kusaidia kutumia simu yako ya android kwa urahisi
App nzuri mpya za Android App nzuri mpya za Android

Karibu tena mwana teknolojia kwenye makala nyingine ya App nzuri za kujaribu kwenye simu ya Android, kumbuka sasa tupo kwenye sehemu ya 17 hivyo kama unataka kujua app nyingine nzuri unaweza kusoma makala nyingine kama hizi na nauhakika utapata kugundua app nyingine nzuri kwaajili ya simu yako ya Android.

Basi bila kupoteza muda twende tukangalia app nzuri za wiki hii, app hizi zitaweza kukusaidia sana kuweza kutumia simu yako ya android kwa namna nzuri na ya kipekee kabisa.

1. WA Direct

WA Direct
Price: Free

WA Direct ni app mpya na nzuri sana kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp, App hii inakupa uwezo wa kumtumia mtu meseji kupitia WhatsApp bila ya kuwa na namba yake kwenye Phonebook yako. Kama unavyojua ili kumtumia mtu meseji WhatsApp ni lazima uwe na namba yake kwenye simu yako na kama ulikua hutaki kufanya hicyo App hii ni nzuri sana kwako.

Advertisement

2. Android Messages

Google Messages
Price: Free

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda kutumia teknolojia kutoka kampuni ya Google basi ni vyema kujaribu App hii pia. App hii ni nzuri sio kwa sababu inatoka kampuni ya Google bali ni kwa sababu ya uwezo wake mpya ambao sasa unaweza kutumia App hii kupitia kompyuta, kifupi ni kuwa sasa utaweza kutuma na kupokea meseji kupitia kompyuta yako kwa kutumia app hii. Unachotakiwa kufanya ni ku-scan bar code kama unavyofanya kwenye WhatsApp.

3. Dumpster: Recover My Deleted Picture & Video Files

App hii ya Dumpster ni app nyingine nzuri sana kwa watumiaji wa simu za Android, App hii inakupa uwezo wa kuzuia kupoteza vitu hasa vile unavyofuta kwa bahati mbaya kwenye simu yako ya Android. Yaani kifupi ni kuwa app hii ni kama vile sehemu ya Recycle Bin kwenye kompyuta yako, ale unapo futa kitu unaweza kukipata ndani ya App hii.

3. Adobe Spark Post

Adobe Spark Post ni app nzuri sana kwa wale wenye akaunti za mitandao ya kijamii kama instagram na mingine. App hii inakupa uwezo wa kutengeneza picha nzuri na nazifu zenye kuweza kufanya akaunti yako ya instagram na akaunti zako nyingine za mitandao ya kijamii kuwa zenye muonekano mzuri.

4. EasyJoin “Essential”- Send photos to PC & more

Easy Join ni app nzuri ya android ambayo inaweza kukusaidia kutuma magaili yako kwa haraka zaidi app hii inakupa uwezo wa kutuma mafile au file mbalimbali kwa kutumia SMS, unaweza kufanya mambo mengi zaidi kwa kutumia app hii unaweza kujaribu app hii kwenye simu yako kujua mengi zaidi.

5. Lumen Privacy Monitor

Lumen Privacy Monitor

Lumen ni app nyongine nzuri na ya mwisho kwenye list hii, app hii inakupa uwezo wa kujua usalama wa simu yako kwa kuonyesha data zinazotumiwa na app zako. App hii inauwezo wa kuonyesha application zako zinatuma wapi data zako na zinapokea data kutoka wapi, unaweza pia kuzuia app hizo kutuma data kwenda kwenye sehemu hizo hivyo hii ni app nzuri sana kama unahisi kuna app huiamini.

Na hizo ndio application zuri za kujaribu kwenye simu yako ya Android, kama umepitwa na application nyingine nzuri za kuedit picha unaweza kusoma list ya app nzuri zilizopita kupitia makala yetu iliyopita. Basi mpaka siku nyingine tena endelea kutembelea Tanzania Tech.

3 comments
  1. Samahani uongozi wa Tt Minilikuwa na tatizo kuwa Facebook yangu na Instagram zimefungiwa siwezi kutumia hizi Account na hizi Account muna mambo yangu mingi pamoja na program zangu nilikuwa naomba kwa uongozi wenu kufunguliwa hizi Account maana ni muhimu kwangu pleas naombeni.

    1. Pole sana, ili kuweza kufunguliwa akaunti zako ni vizuri kuwasiliana na Facebook, pia angalia barua pepe uliyo tumia kujiandikisha nayo kwenye akaunti zako lazima utakuwa umetumiwa ujumbe kwanini akaunti zako zimefungiwa.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use