WhatsApp Imeanza Rasmi Kupambana na Habari za Kuzusha

WhatsApp Kuonyesha Meseji Iliyotoka kwa Mtu Mwingine (Forward Message)
WhatsApp habari za kizushi habari za uongo WhatsApp habari za kizushi habari za uongo

Katika harakati za kupambana na habari za uongo au habari za kuzusha, WhatsApp imekuja na njia mpya ambayo inaweza kuonyesha kama meseji inayosambaa ni ya uzushi. Kupitia blog yake WhatsApp imeandika kuwa hivi karibuni watumiaji wa programu hiyo wataweza kuona kama meseji wanazopokea zimetoka kwa mtu mwingine, yaani kama meseji hiyo ime fowadiwa (forward) kutoka kwa mtu mwingine.

Kama unavyoona kwenye picha hapo juu, meseji zote ambazo zitakuwa zinatoka kwa mtu mwingine zitaweza kuwekewa maneno kwa juu na kuonyesha kwamba ni meseji ambazo ni Forwarded. Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, sehemu hii itakuwa inaonekana kwenye picha, meseji za kawaida ndani ya WhatsApp, Audio na hata pia Video.

Kabla sehemu hii haijatangazwa rasmi WhatsApp ilikuwa ikifanya majaribio ya sehemu hii huko nchini India na nchini Brazil, ambapo ndio inasemekana kunao watumiaji wengi wa programu hiyo, huku pia nchi hizo zikiwa ziko kwa list ya nchi zinazoongoza kwa usambazaji wa habari za uongo au habari za kizushi.

Advertisement

Hivi karibuni kuanzia mwezi May mwaka huu imeripotiwa programu ya WhatsApp imehusishwa na vifo vya watu takribani 12 huko nchini India, huku nchini Brazil programu hiyo ikitumika vibaya kusambaza habari za uvumi kuhusu ugonjwa wa homa ya manjano.

WhatsApp imekua ikijitahidi sana kupambana na habari za uongo au habari za uzushi hadi kufikia hatua ya kuweka matangazo kwenye magazeti ya nchini india ili kuelimisha watu kuhusu kusambaza habari za kizushi au habari za uongo.

Tatizo la kusambaa kwa habari za kizushi au habari za uongo limekuwa ni tatizo la muda mrefu sana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii duniani, ni vizuri sasa kuona baadhi ya mitandao hiyo hiyo imeanza kuchukua hatua za mapema kupambana na habari hizo kuepusha madhara ambayo yanaweza yakawa makubwa zaidi kwa baadae.

Sehemu hii inatarajiwa kuja hivi karibuni kwenye programu zote za WhatsApp za iOS pamoja na Android, hakikisha una sasisha (update) programu yako kuweza kupata sehemu hii.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use