Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sasa Admin Kuzuia Wachangiaji Kupitia WhatsApp Group

admin ataweza kuzuia wachangiaji kutuma meseji mpya kwenye group
Maboresho ya ma-admin WhatsApp Maboresho ya ma-admin WhatsApp

WhatsApp imekuwa ikifanya maboresho kila siku, Hivi karibuni tuligundua kuhusu WhatsApp kuwezesha lugha ya Kiswahili kutumika kwenye App yake, pia tumesikia tetesi mbalimbali za kuhusu mabadiliko kadhaa ya toleo la WhatsApp ya biashara, mabadiliko ambayo inasemekana yataruhusu watumiaji wa programu hiyo kuuza bidhaa kupitia app hiyo.

Tukiachana na hayo yote, hivi karibuni pia WhatsApp imekuwa ikiboresha sehemu ya Magroup hasa kwenye upande wa viongozi wa magroup hayo (Admins) pamoja na njia wanazo tumia kuongoza ma-group hayo.

Advertisement

Mabadiliko makubwa yalianza mara baada ya WhatsApp kuongeza vipengele kadhaa vya kusaidia ma-admin kuweza kuwavua uongozi wa group ma-admin wengine bila kuwaondoa kwenye group. Sasa mara baada ya hilo hatimaye sasa WhatsApp imefanya maboresho zaidi ya ma-admin wa magroup kwa kuleta njia mpya ya ma-admin kuweza kuzuia watu kuchangia kwenye ma-group.

Sehemu hiyo ambayo imeongezwa hivi karibuni inawapa uwezo ma-admin kuzuia wachangia wengine kuandika meseji kwenye group na kuwawezesha ma-admin pekee kuwa na uwezo wa kuongeza meseji kwenye group husika. Sehemu hiyo kwa sasa tayari inapatikana kwenye programu zote za WhatsApp za iOS na Android.

Kama wewe ni Admin na unataka kuwasha sehemu hiyo, unaweza kufanya hivyo kwa kubofya kwenye jina la group (Group Info) kisha shuka mpaka chini kidogo utaona sehemu iliyo andikwa Group Settings kisha chini yake utaweza kuona sehemu iliyoandikwa Send Messages bofya hapo na badilisha kwa kuchagua Only admins. Kwa kufanya hivyo utaweza kuzuia wachangiaji wa kawaida kutuma meseji kwenye group husika na admin pekee ndio atakayeweza kutuma meseji mpya kwenye group husika.

Sehemu hii ni muhimu kwa watu ambao wanataka kuzuia watumiaji kutuma meseji kwa muda fulani kama vile usiku sana au labda wakati fulani ambao admin atakuwa ameamua. Kama nilivyosema, sehemu hii tayari inapatikana kwenye programu ya WhatsApp hivyo kama bado hujapata sehemu hiyo basi hakikisha una sasisha toleo jipya la app ya WhatsApp kupitia Play Store au App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use