Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Habari Zote za Teknolojia kwa Wiki Hii 4/3/2018

Habari kubwa wiki hii ni uzinduzi wa Galaxy S9, Habari nyingine ni..
Hizi Hapa Habari Zote za Teknolojia kwa Wiki Hii 4/3/2018 Hizi Hapa Habari Zote za Teknolojia kwa Wiki Hii 4/3/2018

Habari mwana teknolojia kama wewe ni mpenzi wa teknolojia basi lazima utakuwa unajua kipengele hichi cha tech wiki, kipengele hichi kinakupa mkusanyiko wa habari zote za wiki hii ili iweze kuwa rahisi kwako kujua yote yaliojiri kwenye ulimwengu wa teknolojia kupitia Tanzania Tech. Basi bila kupoteza muda twende tuka-angalie habari zote kubwa za wiki hii kupitia hapa Tanzania Tech.

Wiki hii kampuni ya samsung kupitia mkutano wa MWC 2018 ulio fanyika huko nchini Barcelona, iliziundua simu zake mpya za samsung Galaxy S9 pamoja na Samsung Galaxy S9 Plus. Simu hizo mpya zilikujua na maboresho machache ikiwa pamoja na maboresho makubwa sehemu ya kamera, sehemu ya finger print, aina mpya ya ulinzi pamoja na maboresho mengine madogo madogo.

Advertisement

Kupitia kwenye mkutano huo (MWC 2018) Nokia pia ilizinuda simu zake mpya tano, simu hizo ni pamoja na Nokia 9, Nokia 8 Pro, Nokia 7 Plus, Nokia Banana pamoja na Nokia 4 simu hizi bado hazijatangazwa sitaingia lini sokoni.

Wiki hii ilikuwa ni wiki ya tamasha la MWC 2018, kampuni mbambali za teknolojia zilikuwepo zikionyesha teknolojia zake ikiwa pamoja na kampuni ya Huawei ambayo ilitoa Toleo jipya la Laptop yake ya Huawei Matebook X Pro. Laptop hii inakuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na aina mpya ya kamera iliyo jificha kwenye keyboard.

Kampuni ya magari ya land rover kupitia kwenye mkutano wa MWC 2018 nayo imetangaza ujio wa simu yake ya kwanza inayoitwa Land Rover Explore, simu hii itakuwa ni maalum kwa wasafiri na ni moja kati ya simu ngumu zilizopo mpaka sasa, simu hiyo inategemewa kuingia sokoni hivi karibuni.

Kampuni ya nchini china ZTE nayo ilikuwa kwenye mkutano wa MWC 2018, ambapo ilitangaza ujio wa simu zake mbili mpya za ZTE Blade V9 ambayo inakuja na sifa bora zaidi pamoja na ZTE V9 Vita ambayo inakuja na sifa za kawaida. Simu zote mbili zinategemewa kuingia sokoni mwezi March mwaka huu 2018.

Mtandao wa Youtube kupita blog yake wiki hii ulitangaza ujio wa maboresho ya sehemu ya Live Stream kupitia mtandao wake wa Youtube. Sehemu hizo ni pamoja na kuwepo kwa maoni pembeni ya video za live hata baada ya video hiyo kumalizika. Pamoja na tafsiri ya maneno ya kingereza itakayo kuwa inatokea chini ya video za live na hii ikiwa ni kusaidia watu wengi zaidi kutazama na kuelewa video hizo.

Wiki hii nchini kenya kampuni ya Safaricom kwa kuungana na kampuni ya DOCOMO Digital ya nchini london imefanikisha kuleta huduma ya malipo kwenye soko la Play Store kwa njia ya Mpesa. Huduma hii itawa faidisha watengenezaji wa App nchini humo kwa kuanza kupoka pesa kwenye programu zao kwa njia ya Mpesa. Huduma hiyo inategemewa kuanza siku za karibuni nchini Kenya.

Mtandao wa twitter wiki hii umetangaza kuleta maboresho kadhaa ikiwa pamoja na sehemu mpya ya Bookmark ambayo itamsaidia mtumiaji kuweza kuhifadhi tweet mbalimbali kwaajili ya kusoma baadae. Pia tweet imetangaza ujio wa kitufe kipya cha kushiriki (Share).

Wiki hii, mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA ilimezindua rasmi mfumo wa usajili wa line za simu kwa alama za vidole, mfumo huo utatumika kuhakiki taarifa za wateja mbalimbali wa simu ili kuleta usalama zaidi. Kwa sasa huduma hii inatolewa kwenye baadhi ya sehemu hapa Tanzania pamoja na Zanzibar ikiwa kama sehemu ya majaribio.

Wiki hii Google imatangaza ujio wa Song Maker, tovuti itakayo kusaidia kutengeneza muziki kwa urahisi. Tovuti hii inauwezo wa kukusaidia kutengeneza muziki bila hata ya wewe kutengeneza akaunti au ku-login njia hiyo ni rahisi na inapendeza!.

Na habari ya mwisho kubwa kwa wiki hii ni kuhusu kampuni ya Tigo Tanzania ambayo imeungana na kampuni inayotoa huduma za kifedha ya MasterCard ili kuleta huduma ya Masterpass QR kwa watumiaji wa mtandao wa simu wa Tigo pamoja na Tigo Pesa kwa ujumla. Huduma hiyo itamruhusu mteja wa Tigo kulipa na kupokea malipo kwa urahisi kwa kuscan QR Code maalum.

Na hizo ndio habari kubwa za teknolojia kwa wiki hii iliyoanzia tarehe 25/2/2018, kwa habari zaidi za teknolojia endelea kupitia tovuti ya Tanzania Tech kila siku pia kama unataka kupata habari kwa urahisi unaweza kupakua App yetu ya Tanzania Tech ambayo inapatikana kupitia App Store na Play Store.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use