in

YouTube Kufanya Maboresho ya Sehemu ya Live Streams

Sasa tumia sehemu ya Live Streaming kwa namna ya tofauti

YouTube Live Mubashara

Hivi leo youtube imetangaza kuleta maboresho mapya kwenye sehemu ya Live Stream kupitia mtandao wa Youtube, maboresho hayo yatakuja hivi karibuni ili kuweza kuleta matumizi bora ya mtandao huo hasa sehemu ya Live Streaming au Video Mubashara.

Maboresho yanayo tarajiwa kuja siku za usoni ni pamoja na sehemu mpya ya kuwezesha tafsiri wakati wa Live stream au video mubashara. Sehemu hii itaonekana endepo mtu atakuwa live kupitia channel yake na hapo ndio kutatokea tafsiri ya maneno ya kingereza chini ya video na hii ni ili kusaidia watu wengi zaidi kutoka nchi mbalimbali kuweza kuangalia na kuelewa video hiyo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Maboresho ya pili yanayo tarajiwa kufanyika kwenye sehemu ya video mubashara ni pamoja na sehemu ya maoni. Sasa sehemu ya maoni au maoni yanayo kuwa yanatolewa kwenye video za live yatakuwa yanaonekana hata baada ya video hiyo kuisha. Hapa na maana ya kuwa pale Live Streaming inapo isha na video kuwekwa kwenye mtandao wa youtube basi yale maoni ambayo watu walikuwa wanatoa wakati video ipo live yatakuwa yanaonekana hata baada ya Video hiyo ya mubashara kuisha.

Sehemu nyingine inayo tegemewa kufanyiwa maboresho ni kwa wale ambao wanachukua video za mubashara kupitia simu za mkononi. Sasa watumiaji wa aina hii wataletewa sehemu mpya ambayo itamuwezesha mtumiaji kuweka alama ya mahali alipo chukulia video hiyo yaani hapa na maana ya eneo (Mji au Kitongoji). Sehemu hii itaonekana kwenye video kwa watazamaji na baada ya watazamji kubofya alama au Tag inayo onyesha eneo hilo basi wataletewa video nyingine zilizo rekodiwa kwenye eneo hilo au karibu na eneo hilo.

Sehemu zote hizi zinatarajiwa kuanza kuja siku za karibuni. Hivyo kama wewe ni mtumiaji au unayo channel inayofanya Live Stream mara kwa mara tegemea mabadiliko hayo siku za karibuni.

YouTube Kufanya Maboresho ya Sehemu ya Live Streams
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments