Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Habari za Teknolojia kwa Wiki Hii Tarehe 1/4/2018

Kama ulipitwa na habari kubwa za teknolojia wiki hii soma hapa
Habari za Teknolojia Habari za Teknolojia

Habari mwana teknolojia na heri ya sikukuu ya pasaka, bila shaka unaendelea vizuri na bado unafuatilia teknolojia kwa ukaribu zaidi. Kama ulipitwa na habari kubwa za teknolojia wiki hii basi hii ndio sehemu ambayo ninaenda kukujuza yote yaliojiri kwa upande mzima wa teknolojia. Basi bila kupoteza muda twende nikakujuze habari zote kubwa za teknolojia zilizotokea kwa wiki hii.

Habari kubwa pengine kuliko zote kwa wiki hii ni kuhusiana na uzinduzi wa simu mpya za Huawei, simu ambazo zilikuwa gumzo sana kutokana na kuja zikiwa na kamera tatu kwa nyuma. Huku toleo maalum la Huawei Porsche likija na ukubwa wa ndani wa GB 512.

Advertisement

Habari nyingine kubwa kwa upande wa teknolojia wiki hii, ni kuhusiana na taarifa iliyotolewa na Google kuhusu kufungia baadhi ya simu ambazo hazijawa Certified. Kufungia huku kutahusisha kutoweza kutumia programu za Google kama vile soko la Play Store, Google Maps na programu nyingine kama hizo. Kuangalia kama simu yako iko Certified ingia kwenye soko la Play Store kisha bofya Settings > kisha angalia mwisho wa ukurasa huo.

Habari nyingine ni kuhusu kampuni ya tecno ambayo inasemekana kujiandaa na uzinduzi wa simu yake mpya ya Tecno Camon X ambayo inasemekana kuwa na maboresho zaidi kwenye upande wa kamera. Simu hii inategemewa kuzinduliwa huko Nigeria siku ya alhamisi ya tarehe 5 mwezi huu.

Wiki hii pia kampuni ya Apple ilikuwa kwenye vichwa vya habari za teknolojia kutokana na kufanya tamasha lake linalohusu maswala ya elimu ikiwa pamoja na kuzindua iPad mpya ya inch 9.7 inayo tumia kalamu ambayo itakuwa maalum kwaajili ya wanafunzi.

Wiki hii pia sakata la Facebook kuvujisha data za watumiaji zaidi ya Milioni 50 kupitia kampuni ya Cambridge Analytical bado liliendelea na wiki hii waziri mkuu wa zamani wa kenya Raila Odinga alisema kuwa ataishtaki kampuni ya Facebook na Cambridge Analytical kutokana Facebook pamoja na kampuni ya Cambridge Analytica kwa kutumia jina lake kuendesha kampeni ya kuchochea uhasama wa kikabila kwa lengo la kuhujumu azma yake ya kuwa rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017.

Katika hali ya kuendelea kwa sakata hilo la Facebook na Cambridge Analytical, Kampuni ya Playboy ambayo ina miliki jarida la Playboy magazine nayo wiki hii imejitoa kwenye mtandao wa facebook kutokana na kuona kuwa mtandao huo bado sio salama.

Nchini misri wiki hii mambo yamekuwa tofauti wakati serikali ikizindua rasmi mtandao wake wa kwanza wa kijamii ambao unafanana kabisa na facebook. Kwa sasa mtandao huo unapatikana kupitia anuani ya egface.com na tayari kuna watumiaji wa chache kutoka nchini humo wamesha anza kutumia mtandao huo.

Wiki hii kampuni ya Apple ilizindua toleo jipya la iOS 11.3 ambalo linakuja kuja na maboresho kadhaa huku maboresho makubwa yakiwa ni maboresho ya battery. Maboresho mengine ni madogo madogo na kwa sasa toleo hilo linapatikana hivyo unaweza kupakua toleo hilo kwenye kifaa chako.

Wiki hii Google kupitia ukurasa wa Blog yake imeandika kuwa, kuanzia tarehe 30 mwezi huu google haitakuwa inaboresha tena tovuti ya Google URL Shortener na pia kuanzia tarehe 13 ya mwezi wa nne watu ambao tayari walishakuwa wanatumia tovuti hiyo ndio watakao weza kuendelea kutumia tovuti hiyo. Kwa wale ambao hadi kufika tarehe 13 Aprili 2018 watakuwa bado hawaja anza kutumia tovuti hiyo basi hawato weza kutumia tovuti hiyo kabisa.

Na hizo ndio habari kubwa za teknolojia kwa wiki hii nzima, kama ulipitwa na habari za teknolojia kwa wiki iliyopita unaweza kusoma habari hizo hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, mpaka wiki ijayo nakutakia HERI YA PASAKA.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use