Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

App Nzuri Soko Maalum Kwaajili ya Kutambua Application Nzuri

Sasa utaweza kutangaza app yako kwa urahisi bila kulipia.
App Nzuri Soko Maalum Kwaajili ya Kutambua Application Nzuri App Nzuri Soko Maalum Kwaajili ya Kutambua Application Nzuri

Ukweli ni kwamba, siku hizi karibia kila siku wabunifu wa programu hapa Tanzania huweka programu zao kwenye masoko mbalimbali. Hii ikiwa ni pamoja na masoko ya Play Store, App Store, Windows Store pamoja na masoko mengine mbalimbali.

Lakini pamoja na kuwepo kwa masoko hayo maarufu kama Play Store, bado imekuwa ni ngumu sana kwa app za kitanzania kuweza kuonekana na watanzania hasa uki zingatia soko la Play Store lina apps takribani milioni 2.87 hadi kufikia mwezi March mwaka huu 2020. Hii ni sawa na kusema kila siku app zaidi ya 3,739 huwekwa kwenye soko la Play Store pekee, hii ni kwa mujibu wa tovuti ya appinventiv.com.

Advertisement

App Nzuri Soko Maalum Kwaajili ya Kutambua Application Nzuri

Sasa kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya apps ambazo huwekwa kwenye masoko hayo, ni wazi kuwa wote tunahitaji kupata sehemu moja ya kitanzania ambayo itasaidia kuweza kutangaza app za kitanzania na apps nyingine bora.

Karibu App Nzuri..!

Tanzania Tech tunakuletea tovuti mpya ya App nzuri, tovuti hii ina lengo la kusaidia watumiaji wa programu pamoja na wabunifu wa programu kuweza kutangaza programu zao kwa urahisi na haraka.

App Nzuri Soko Maalum Kwaajili ya Kutambua Application Nzuri

Kupitia tovuti hii utaweza kujua programu au app nzuri 10 kila siku ikiwa pamoja na kuweza kupakua programu hizo kwa urahisi kupitia simu au kompyuta yako. Kwa upande wa wabunifu wa programu wa kitanzania wataweza kuweka programu zao kwa kuomba ziwekwe kwenye tovuti hii bila kulipia gharama yoyote. Hii italeta urahisi kwa watumiaji kujua programu zao pamoja na kuweza kuzipakua kwa wingi.

Kupitia tovuti hii utaweza kupata fomu maalum ambayo itakusaidia kuweza kuweka app yako kwenye tovuti hii kwa haraka na urahisi. Pia hata kama wewe sio mbunifu wa programu na unajua app yoyote nzuri pia unaweza kutumia fomu hiyo kuweza kutujulisha kuhusu app hiyo. App hiyo itawekwa kwenye tovuti yetu moja kwa moja baada ya kupitia ukaguzi maalum ambao utafanyika baada ya siku moja.

App Nzuri Soko Maalum Kwaajili ya Kutambua Application Nzuri

App zote zitawekwa kwenye tovuti hii kila baada ya siku moja ya kazi. Mbali ya hayo kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kujaribu app mpya kwenye kifaa chako cha Windows, Android, iOS, macOS au Linux basi unaweza kutembelea tovuti hii kila siku kwani utaweza kuona app mpya 10 kila siku ambazo huweza ulikuwa huzijui kwa namna moja ama nyingine. Pia utaweza kupakua app hizo kwa kupelekwa kwenye link husika moja kwa moja.

Hii ni nafasi yako kwako wewe mbunifu wa programu kuweza kutangaza app yako na pia ni nafasi yako wewe mpenzi wa app mbalimbali kuweza kupata nafasi ya kujua app nzuri kila siku kupitia kifaa chako. Unaweza kutembelea tovuti hii mpya kwa kubofya hapo chini. Karibu sana kwenye ulimwengu wa App nzuri.

Tembelea App Nzuri Hapa

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use