Australia Yazindua App ya Kutambua Wagonjwa wa Corona

App hii itasaidia kujua kama mtu aikaribiana na mwenye virusi hivyo kwa muda mrefu
Australia Yazindua App ya Kutambua Wagonjwa wa Corona Australia Yazindua App ya Kutambua Wagonjwa wa Corona

Serikali ya Australia imetangaza uzinduzi wa App mpya ya COVIDSafe app ambayo inasemekana kuwa na uwezo wa kutambua wagonjwa wa corona kwa kutumia smartphone.

App hiyo mpya ambayo imezinduliwa hapo jana, hadi sasa tayari imesha pakuliwa kwa zaidi ya mara milioni moja huku raia wa nchi hiyo wakionyesha kufurahia kuwepo kwa app hiyo. Kwa mujibu wa tovuti ya BBC, App hiyo ya COVIDSafe inatumia mfumo maalum wa Bluetooth ambao huweza kuhifadhi data pale mtu anapo karibiana na mwengine kwa zaidi ya mita 1.5 au Futi 4.9.

Baadae data hizo huifadhiwa kwa usalama kwenye server za serikali na endapo mmoja kati ya watu walio karibiana watagundulika kuwa na virusi vya corona basi watumiaji wote walio karibiana na mtu huyo kwa muda wa zaidi ya dakika 15 watapewa taarifa moja kwa moja kupitia app hiyo.

Advertisement

Australia Yazindua App ya Kutambua Wagonjwa wa Corona

Kwa mujibu wa tovuti ya BBC, hadi siku ya jana taarifa hizo zilipo chapishwa Australia ilikuwa na watu 6,694 walio thibitishwa kuambukizwa virusi vya corona, na vifo 80 vinavyo tokana na virusi hivyo vya Corona au COVID-19.

Unapo jisajili kwenye App hiyo unatakiwa kujaza fomu maalum ambayo itakuhitaji kujaza vitu sahihi kama vile Jina Kamili, Namba ya simu, Mahali mtumiaji anapoishi, ikiwa pamoja na umri kamili wa mtumiaji.

Hata hivyo, Serikali ya Australia imesema data hizo zitahifadhiwa kwa muda wa masaa 21 na pia sata hizo hufutwa pale tu mtumiaji atakapo futa app hiyo kutoka kwenye simu yake. App hiyo inapatikana kwa wananchi wa nchini Australia na inapatikana kwenye mifumo yote ya Android na iOS.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use