Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Google Meet Njia Mpya ya Kufanya Mikutano Kwa Video

Njia mpya ya kufanya mikutano kwa njia ya video kupitia Google
Google Meet Njia Mpya ya Kufanya Mikutano Kwa Video Google Meet Njia Mpya ya Kufanya Mikutano Kwa Video

Wakati dunia ikizidi kupambana na Virusi vya Corona (COVID-19), teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video inazidi kukuwa kwa kasi sana kiasi kwamba kampuni nyingi za teknolojia sasa zinakuja na teknolojia hizo ili kuwezesha watu kuwasiliana kwa urahisi hasa kipindi hichi ambacho watu wanashauriwa kuepuka mikusanyiko ya watu wengi.

Google ni moja ya kampuni ambazo hivi karibuni zilitangaza kuja achia njia mpya ya kuwasiliana kwa njia ya video kupitia programu yake ya Google Meet. Kama ulikuwa hujui, Google Meet hii ni sehemu ambayo ilikuwa ya kulipia kwa watumiaji wa Google Business, lakini sasa imeletwa kwa watumiaji wote bure kabisa. Kupitia Google meet mtu yoyote ataweza kuwasiliana kwa njia ya video na watu 50 kwa wakati mmoja kwa pamoja.

Advertisement

Kupitia Google Meet utaweza kutengeneza mkutano kwa urahisi kwa kutumia app ya Android au iOS, au kama hutaki kutumia programu hizo unaweza kutengeneza mkutano kwa urahisi kwa kutembelea tovuti ya meet.google.com. Sio lazima kuwa na app au sio lazima watu unaotaka kuchat nao kwa njia ya video wawe na programu hiyo, bali kitu cha muhimu wanatakiwa kuwa na internet pamoja na link ya mkutano ambayo utakuwa umeipata mara baada ya kutengeneza mkutano kupitia app au tovuti ya Google Meet.

Pia kama unatumia app ya Gmail unaweza kuapa sehemu ya Meet moja kwa moja kupitia Email yako na hapo utaweza kutengeneza mikutano kwa urahisi na haraka.

Google Meet Njia Mpya ya Kufanya Mikutano Kwa Video

Hivi karibuni njia ya video imekuwa ikitumika sana kufanya mikutano kwa watu mbalimbali, hii ni baada ya marufuku ya kukusanyika iliyokuja baada ya kuanza kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona ambayo yalianza kuripotiwa tokea mwishoni mwa mwaka jana 2019.

Mbali na Google Meet, Facebook nayo imepanga kuja na sehemu mpya ya Rooms, sehemu ambayo itasaidia watu kufanya mikutano kwa njia ya video. Sehemu hiyo mpya ya Rooms itakuwa inapatikana kwenye mitandao yake yote ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Messenger. Ambapo pia ili kutumia sehemu hiyo huna haja ya kuwa na programu nyingine yoyote.

Sehemu ya Rooms imeanza kupatikana tayari kwa watumiaji wa nchi mbalimbali kwenye mitandao ya Messenger pamoja na Facebook huku sehemu hiyo ikiwa inategema kufika kwenye programu za Instagram na WhatsApp baadae mwaka huu. Kwa sasa sehemu hii bado haijafika Tanzania hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza pindi sehemu hiyo itakapo anza kupatikana rasmi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use