Hatimaye Apple Yaleta Huduma ya Apple Music Nchini Tanzania

Sasa download na sikiliza nyimbo zaidi ya milioni 60 ukiwa Tanzania
Hatimaye Apple Yaleta Huduma ya Apple Music Nchini Tanzania Hatimaye Apple Yaleta Huduma ya Apple Music Nchini Tanzania

Kampuni ya Apple, hivi leo imetangaza kupanua upatikanaji wa huduma zake kwenye nchi mbalimbali ikiwemo huduma ya Apple Music ambayo kuanzia leo itakuwa inapatikana pia hapa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Apple, huduma nyingie ambazo zimepanuliwa ni pamoja na huduma za Apple Arcade, Podcasts na iCloud ambazo zote zitakuwa zinapatikana barani afrika kwenye nchi za Cameroon, Côte d’Ivoire, Democratic Republic of the Congo, Gabon, Libya, Morocco, Rwanda, pamoja na Zambia. Hapo awali huduma hizo hazikwepo kwenye nchi hizo.

Mbali na huduma hizo, huduma ya Apple Music ambayo hutoa huduma ya kusikiliza nyimbo mbalimbali kutoka kwa wasanii maarufu kote duniani sasa itakuwa inapatikana kwa nchini Tanzania ikiwemo pamoja na nchi nyingine za Algeria, Angola, Benin, Chad, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Mozambique, Namibia, Republic of the Congo, Senegal, Seychelles, Sierra Leone, pamoja na Tunisia.

Advertisement

Kupitia Apple Music ambayo inasemekana kuwa na nyimbo zaidi ya Milioni 60, utaweza kusikiliza nyimbo mpya kutoka Afrika ikiwa pamoja na kusikiliza nyimbo unazo zipenda kutoka kwa wasanii wakubwa kutoka ndani na nje ya Tanzania ikiwa pamoja na Playlist za Kiafrika kama Afrobeat, Africa Now na nyingine nyingi.

Hatimaye Apple Yaleta Huduma ya Apple Music Nchini Tanzania

Kwa sasa Apple Music inapatikana kwa watumiaji wote wa Android, iOS, iPad OS, MacOS pamoja na watumiaji wa Windows. Kama unatumia kompyuta unaweza kuangalia ndani ya iTunes unaweza kuona kipengele cha Apple Music. Pia vilevile kwa sasa kama upo afrika Apple imetoa ofa na utaweza kusikiliza muziki na kudownload bure kwa muda wa miezi sita na baada ya hapo utalipia Tsh 7000 kila mwezi kwa mtu mmoja na Tsh 11,000 kwa watu zaidi ya sita.

Hatimaye Apple Yaleta Huduma ya Apple Music Nchini Tanzania

Kama unataka kujaribu Apple music kwenye simu yako ya Android basi unaweza kupakua app hiyo kupitia link hapo chini na moja kwa moja utaweza kusikiliza na kudownload muziki kwa urahisi. Kwa sasa bado hakuna taarifa kama wasanii wa kitanzania wanaweza kuweka nyimbo zao kwenye soko la Apple music ila ni wazi kuwa kutokana na huduma hii kufika hapa Tanzania basi ni wazi kuwa uwezo huo lazima utakuwa unapatikana. Japo kuwa sina uhakika!

Apple Music
Price: Free
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use