Instagram Kuja na Profile Maalum Kwaajili ya Walioaga Dunia

Sasa utaweza kutambua akaunti za Instagram za watu walioaga Dunia
Instagram Kuja na Profile Maalum Kwaajili ya Walioaga Dunia Instagram Kuja na Profile Maalum Kwaajili ya Walioaga Dunia

Instagram ni moja kati ya mtandao unaotumiwa zaidi hasa hapa Tanzania, kutokana na mtandao huo kuendelea kutumika na watu wengi, baadhi ya watu hutumia mtandao huo kupata habari za marafiki na jamaa ambao inawezekana umepoteza nao kwa muda mrefu.

Lakini kuna wakati unakuta kwa bahati mbaya marafiki au jamaa wa karibu wamepoteza maisha kwa muda mrefu bila ya wewe kujua au kupata taarifa. Ndio maana Instagram imetangaza kuja na aina mpya ya profile mpya inayoitwa Remembering.

Remembering ni profile ambayo itakuwa maalum kwa watumiaji wa instagram walioaga dunia. Profile hii itasaidia watumiaji kuweza kubakia na kumbukumbu za wapendwa wao ikiwa pamoja kuwafahamisha watu wengine kama profile hiyo ilikuwa ya mtu aliye aga dunia

Advertisement

Instagram Kuja na Profile Maalum Kwaajili ya Walioaga Dunia

Kama unavyoweza kuona hapo juu, profile ya mtu aliye aga dunia itakuwa na maneno “Remembering” maneno ambayo yatakuwa yana ashiria mtu huyo hayupo tena duniani. Hata hivyo inasemekana kuwa baada ya profile hiyo kubadilishwa na kuwa hivyo, hakuna mtu yoyote ambae ataweza kubadilisha kitu chochote kwenye profile hiyo kwa namna yoyote.

Mbali na mtu kubadilisha kitu, pia inasemekana hakuna mtu ambaye atakuwa na uwezo wa kuandika maoni yoyote mapya kwenye picha zilizopo ikiwa pamoja na kuingia kwenye profile hiyo au ku-login kwa namna yoyote. Pia profile hiyo itaondolewa kwenye sehemu ya Explore, hivyo hakuna mtu yoyote ambaye ataweze kupata profile hiyo kwa kutumia sehemu hiyo. Njia pekee itakua ni kuwa na link au username ya moja kwa moja kwenye profile hiyo.

Kwa sasa Instagram imetangaza kuwa profile hiyo bado ipo kwenye hatua za majaribio, lakini tayari ipo njia ambayo unaweza kutuma maombi kurasa ya mpendwa wako iwekewe alama hiyo ya “Remembering”. Unaweza kufanya hivyo kwa kujaza fomu maalum iliyopo kwenye tovuti ya Instagram hapa. Kumbuka kujaza fomu hiyo unatakiwa kuwa na ushahidi kama mtu huyo ameaga dunia ikiwa pamoja na majina yake kamili pamoja na tarehe aliyo aga dunia.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use