in

Apple Yasitisha Programu ya iTunes na Kuleta Programu Mpya 3

Sasa programu hiyo imetenganishwa na kuwa apps tatu tofauti

Apple Yasitisha Programu ya iTunes na Kuleta Programu Mpya 3

Kama ilivyo semekana kwenye tetesi, hatimaye kampuni ya Apple imetangaza kupitia mkutano wa WWDC kuwa programu ya iTunes haito kuwepo tena na badala yake kutakuwa na programu nyingine tatu ambazo zitafanya kazi ambazo iTunes ilikuwa inafanya.

Hapo awali programu ya iTunes ilikuwa ndio programu inayotumika kufanya mambo mbalimbali kama vile kuweka muziki baina ya kompyuta na simu au iPod, Kusikiliza muziki mtandaoni pamoja na kuangalia vipindi au filamu mtandaoni.

Sasa yote hayo yanaenda kubadilika kwani Apple imetangaza kuwa, kazi zote hizo zitaenda kufanywa na programu nyingine, kwa mfano kazi ya kuweka muziki baina ya simu na kompyuta itafanywa na sehemu mpya ndani ya mfumo wa macOS, kwa upande wa kusikiliza muziki kazi hiyo itafanywa na programu ya Music, huku kazi ya kusikiliza vipindi vya mtandaoni ikifanywa na programu ya Podcast. Pia kama utakuwa unatafuta filamu utaweza kuzipata kupitia Apple TV.

Apple Yasitisha Programu ya iTunes na Kuleta Programu Mpya 3

Hata hivyo kwa upande wa Windows bado haijajulikana kama programu ya iTunes itaendelea kufanya kazi au kama kampuni ya Apple itakuja na suluhisho lingine. Hata hivyo programu zote zitakuja zikiwa ndani ya mfumo mpya wa macOS Catalina ambao umezinduliwa rasmi hapo siku ya jana.

Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted

Kama unataka kujua zaidi kuhusu mfumo mpya wa macOS Catalina, hakikisha unasoma makala inayofuata. Kwa habari zaidi kuhusu mkutano wa WWDC na yote yaliyojiri hakikisha unatembelea ukurasa wetu wa #WWDC 2019 Hapa.

Written by Jackline John

Jack ni mpenzi wa teknolojia napenda kuandika kuhusu maujanja, simu na kompyuta. Unaweza kunipa maujanja kupitia [email protected]

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.