in

Facebook Kuja na Aina Mpya ya Reaction ya ‘Care’

Sasa utaweza kuonyesha kama unajali kupitia facebook na messenger

Facebook Kuja na Aina Mpya ya Reaction ya ‘Care’

Facebook imetangaza kuwa inatarajia kuja na aina mpya ya reaction kwenye tovuti yake ya Facebook.com pamoja na app zake za mifumo ya Android na iOS, aina hiyo mpya ya reaction inalenga hasa kipindi hichi ambacho dunia ina pambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Kwa mujibu wa Facebook, reaction hiyo mpya ambayo itakuwa inaitwa “care” itakuwa sambamba na reaction nyingine kwenye mtandao huo kuanzia wiki ijayo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Facebook Kuja na Aina Mpya ya Reaction ya ‘Care’

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, reaction ya care inategemea kuonekana kama ilivyo kwenye picha hapo juu, kwa upande wa facebook utaweza kuona emoji iliyo kumbatia love na kwa upande wa messenger utaweza kuona reaction ya care ikiwa na muonekano wa moyo (love) inayodunda.

Mbali na mabadiliko hayo ya reaction, facebook pia inategemea kuja na sehemu mpya ambayo itakuwa ikionyesha alama kwenye link zinazo sambazwa kwenye mtandao huo zenye taarifa za uongo kuhusu virusi vya corona au COVID-19. Sehemu hiyo mpya tayari imesha anza kufanya kazi kwenye mtandao wa facebook na unaweza kuiona pale unapo ona link ya maelezo ya uongo kuhusu virusi vya corona.

Facebook Kuja na Aina Mpya ya Reaction ya ‘Care’

Infinix Yashinda Tuzo za Design Kimataifa (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.