Katika ulimwengu huu wa sasa ni wazi kuwa watu wengi sana hupendelea kuangalia TV kupitia kwenye simu kuliko hata kuangalia TV wakiwa nyumbani. Hii inatokana na kuwa watu wengi zaidi humiliki simu kuliko hata TV zenyewe.
Kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kuangalia TV au IPTV kupitia simu yako ya mkononi. Kizuri ni kuwa, pia unaweza kuchukua list ya TV hizi na kuweka kwenye app mbalimbali bure kabisa bila kulipia, TV hizi au IPTV hizi huongezwa kila wakati hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi ku-update bali ni kutumia tu, bure bila kikomo.
Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja kama wewe ni mtumiaji wa kawaida (sio developer kwa debeloper angalia mwisho wa makala hii ) na ungependa kuangalia TV tu basi fuata maelekezo haya mafupi.
Kwa kuanza download app kupitia link hapo juu, baada ya kudownload fungua app hiyo kisha endelea kwa kufuata maelezo hapo chini.
Baada ya kupakua app hapo juu, bofya hapo chini kisha utapelekwa kwenye link yenye channel zaidi ya 5000+ ambazo unaweza kuangalia kwa kutumia app uliyo download hapo juu.
Baada ya hapo copy link hiyo kisha bofya alama ya jumlisha kwenye app uliyo download kupitia link ya mwanzo kwenye ukurasa huu.
Baada ya kubofya alama ya jumlisha iliyopo juu upande wa kulia, moja kwa moja itatokea sehemu ambayo unatakiwa kupaste link uliyopata hapo juu mara baada ya kubofya kitufe cha Copy Link. paste link hiyo kwenye sehemu iliyo andikwa Playlist URL kisha bofya OK.
Baada ya hapo kama unatumia data ya simu yako moja kwa moja utaweza kuona maandishi kama hayo hapo chini, weka alama ya tiki kisha bofya Continue.
Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona channel nyingi zikiwa zimetokea kwenye ukurasa wa all na unaweza kutafuta channel kulingana na category, pia unaweza kutafuta jina la channel kama unataka kupata channel ambayo unaijua.
Kupitia njia hii utaweza kupata channel nyingi sana ambazo unaweza kuangalia kwenye simu yako bila kulipia. Kumbuka ili kuangalia channel hizi unatakiwa kuwa na data kwenye simu yako, mbali na hayo kama wewe ni developer na unataka kuchukua channel hizi na kuweka kwenye app yako basi moja kwa moja unaweza kudownload file lenye channel hizi kupitia link hapo chini.
Mapaka hapo natumaini utakuwa umeweza kuangalia channel zaidi ya 5000+ kupitia simu yako ya mkononi, pia kama wewe ni developer natumaini sasa upo kwenye hatua za awali kuweza kuweka app yako ya TV kupitia soko la play store.