Kampuni ya Infinix hivi leo April 24 imezindua toleo jipya la simu zake za GT 50 Pro, simu ambazo ni maalum kwa ajili ya wapenzi wa Game.
Toleo hili linakuja na maboresho mapya ikiwa pamoja na chipset ya MediaTek Dimensity 8400 Ultimate yenye uwezo wa hadi GHz 3.25, huku ikisaidiwa na CPU ya Octa-core (1×3.25 GHz Cortex-A725 & 3×3.0 GHz Cortex-A725 & 4×2.1 GHz Cortex-A725), pamoja na GPU ya Mali-G720 MC7. Simu hii pia inakuja na sehemu maalum ya kupooza CPU kwa ajili ya kuwezesha kucheza game kwa muda mrefu bila simu kupata moto.

Kwa upande wa RAM, Infinix GT 50 Pro inakuja na chaguo moja la RAM ya GB 12, pamoja na uwezo wa uhifadhi wa ndani (Storage) ya GB 256 au GB 512. Uhifadhi huu unatosha kuweka game za kutosha kwa watumiaji wengi, hivyo simu hii haina sehemu ya kuongeza uhifadhi kwa kutumia memory card.
Mbali ya hayo, kwa upande wa camera GT 50 Pro inakuja na kamera mbili kwa nyuma, huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 50 na nyingine ikiwa na Megapixel 8, tofauti na toleo la mwaka jana lenye kamera kubwa zaidi.

Kwa upande wa Kamera ya mbele ya simu hii inakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K kwa kutumia kamera yake yenye uwezo wa Megapixel 13.
Kwenye upande wa chaji Infinix GT 50 Pro inakuja na battery ya Li-Ion yenye uwezo wa 6150 mAh au 6500 mAh. Ukubwa huu wa battery unaweza kusaidia simu hii kudumu na chaji siku nzima kulingana na matumizi.

Mbali ya yote simu hii inakuja na sehemu nyingi za kuwezesha kutumia simu hii maalum kwa ajili ya game. Mfano wa sehemu hii ni kuwepo wa cooling system, vitufe maalum kwa ajili ya kurahisha pale unapo cheza game na sehemu nyingine nyingi.
Kwa upande wa bei tegemea kuipata Infinix GT 50 Pro kwa kuanzia TZS 1,350,000 hadi TZS 1,500,000.


