Bidhaa za Apple

Je Hii Ndio Tarehe ya Kutoka kwa Bidhaa Mpya za Apple?

Msimu wa spring unakaribia uko marekani, huu ni wakati maalumu kwa kampuni ya simu za mkoni Apple kutoa matoleo mapya ya bidhaa zake kama iPhone, iPad na watch band, hayo yamedhibitishwa na blog ya marekani  iitwayo 9to5 Mac.

Tarehe 15 March siku ya jumanne mwaka 2016 ni tarehe maalumu kwa kampuni hiyo ya Apple kwani, ndio siku kampuni hiyo itakua ikizindua bidhaa zake mpya za iPhone, iPad na watch band taarifa zinaendelea kusema kutoka blog ya 9to5 Mac.

Hata hivyo blog hiyo inaendelea kusema kua Apple itatoa bidhaa zake mpya kama vile 4– inch iPhone 5SE na iPad Air 3.

Simu zote mpya zita jumuisha uongezaji wa ubora wa kamera na kuongezwa kwa application kadhaa katika vifaa hivyo, hata hivyo blog hiyo maarufu marekani inasema kuwa iPad Air 3 itakuwa na kamera nzuri ya nyuma itakayokua na ubora zaidi kuliko matoleo yake ya nyuma ya iPad. Na pia kwa upande wa watch band Apple itaongeza rangi nyingi mbalimbali pamoja na kuweka mikanda ya plastic kwenye saa hizo maharufu kama watch band. Kampuni ya Apple haikutoa maoni yoyote kuhusiana na taarifa hizi.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Je Unatumia iPhone Iliyovunjika Kioo? Soma Hii 1
Je Unatumia iPhone Iliyovunjika Kioo? Soma Hii
Next Post
whatsapp emoj

Whats App Yatoa Mabadiliko Mapya ya Emojis