Hizi Hapa Simu Mpya za Honor 600, 600 Pro na 600 Lite 1

Hizi Hapa Simu Mpya za Honor 600, 600 Pro na 600 Lite

Simu zote zinakuja na sifa bora huku Honor 600 Pro ikiwa na sifa bora zaidi

Kampuni ya Honor imekuwa ni kinara wa simu za daraja la kati kwa muda mrefu, hivi karibuni kampuni hiyo imezindua matoleo mapya ya simu zake za Honor 600 ambayo inajumisha Honor 600, 600 Pro na 600 Lite.

Hizi Hapa Simu Mpya za Honor 600, 600 Pro na 600 Lite 2

Sifa na Bei

Simu zote zinakuja na sifa bora huku Honor 600 Pro ikiwa na sifa bora zaidi, kwa kuwa na chipset ya Snapdragon 8 Elite huku ikisaidiwa na RAM ya GB 12, huku Honor 600 ikiwa na chipset ya Snapdragon 7 Gen 4, 600 Lite ikiwa na Dimensity 7100 Elite na RAM kati ya GB 8 au GB 12.

Kwa upande wa storage simu hizi zinakuja na machaguo tofauti kati ya GB 256GB/512GB/1TB kwa 600 Pro, na 128GB/256GB/512GB kwa Honor 600, pamoja na 128GB/256GB kwa Honor 600 Lite.

Kwa upande wa kamera, 600 Pro inakuja na kamera za nyuma tatu Megapixel 200, Megapixel 50 na Megapixel 12. Huku ikiwa na kamera moja ya selfie ya Megapixel 50.

Honor 600 Pro

TZS 2,850,000
Honor 600 Pro
CPU Octa-core (2x4.32 GHz Oryon V2 Phoenix L + 6x3.53 GHz Oryon V2 Phoenix M)
RAM 12GB
Storage 256GB/512GB/1TB
Display AMOLED, 6.57 inches
Camera Triple 200 MP, 50 MP, 12 MP
OS Android 16
Rating 7 / 10

Honor 600 inakuja na kamera mbili za nyuma zenye Megapixel 200, na Megapixel 12. Huku ikiwa na kamera ya selfie ya Megapixel 50.

Honor 600

TZS 1,900,000
Honor 600
CPU Octa-core (1x2.8 GHz Cortex-720 & 4x2.4 GHz Cortex-720 & 3x1.8 GHz Cortex-520)
RAM 8/12GB
Storage 128GB/256GB/512GB
Display AMOLED, 6.57 inches
Camera Dual 200 MP, 12 MP
OS Android 16
Rating 6.8 / 10

Toleo la Honor 600 Lite linakuja na kamera mbili za nyuma yaani Megapixel 108, na Megapixel 5, pamoja na kamera ya selfie ya Megapixel 16.

Honor 600 Lite

TZS 1,080,000
Honor 600 Lite
CPU Octa-core (4x2.4 GHz Cortex-A78 & 4x2.0 GHz Cortex-A55)
RAM 8/12GB
Storage 128GB/256GB
Display AMOLED, 6.6 inches
Camera Dual 108 MP, 5 MP
OS Android 16
Rating 6.8 / 10

Kwa upande wa upatikanaji tarajia kupata Honor 600 Pro kuanzia TZS 2,850,000 hadi TZS 3,000,000. Honor 600 Kuanzia TZS 1,900,000 hadi 2,000,000, na 600 Lite kuanzia TZS 1,080,000 hadi TZS 1,150,000.

Comments

2
  • Dalali Mkononi
    Dalali Mkononi

    Hii kali sana naweza kupata wapi hizi simu kwani zimeshakuja hapa Tanzania

  • Fotunatus Moshi
    Fotunatus Moshi

    Hii itakuja Tanzania kweli..?

See all 2 comments
Previous Post
Kampuni ya Asus Kusitisha Uzalishaji wa Smartphone 3
Kampuni ya Asus Kusitisha Uzalishaji wa Smartphone