Zifahamu Hizi Hapa Apps Nzuri Kwa ajili ya Afya ya Akili

Jiweke salama kwa kufahamu kuhusu Afya ya Akili kwa kutumia App hizi nzuri
Zifahamu Hizi Hapa Apps Nzuri Kwa ajili ya Afya ya Akili Zifahamu Hizi Hapa Apps Nzuri Kwa ajili ya Afya ya Akili

Kwanza napenda ufahamu kuwa mimi sio daktari na wala sina ujuzi wowote kwenye maswala ya Afya au Afya ya Akili kwa ujumla, lakini pamoja na hayo naweza kusema kuwa nina ujuzi kidogo wa maswala ya teknolojia na hivyo naweza kukushauri mambo machache ambayo yako ndani ya uwezo wangu.

Japokuwa nilipokuwa mdogo nilitamani kuwa daktari, lakini maisha yamenipeleka sehemu nyingine kama wengi wenu hapa.

Hivyo basi, napenda ufahamu kuwa ushauri ulipo hapa ni ushauri kwa upande wa teknolojia tu, hivyo ni muhimu kuhakikisha una muona daktari kama unajihisi unalo tatizo lolote ambalo linaweza kuathiri maisha yako au ya watu walio kuzunguka.

Advertisement

Basi baada ya kusema hayo basi moja kwa moja twende kwenye makala hii ambayo itakusaidia kujua apps nzuri ambazo zinaweza kusaidia afya yako ya akili kwa namna moja ama nyingine.

Ada

Ada ni moja kati ya app bora sana kwa Afya pamoja na afya ya akili, app hii inatumia mfumo maalum ambao unaweza kukusaidia kuweza kujua dalili mbalimbali za magonjwa ya kawaida ikiwa pamoja na magonjwa ya msongo wa mawazo. Uzuri wa app hii ni kuwa inapatikana pia kwa lugha ya kiswahili hivyo unaweza kupata ushauri kwa lugha unayo ielewa kwa asilimia 100.

eMoods Bipolar Mood Tracker

eMoods ni app nyingine ambayo itakusaidia sana kufahamu mengi kuhusu afya yako ya akili, app hii inauwezo wa kusaidia kujua mihemuko yako au mood ya kila siku. Kupitia app hii utaweza kujaza jinsi unavyo jisikia kila siku na hii itasaidia kutengeneza ripoti ambayo itakuonyesha mihemuko yako inasababishwa na nini.

Wysa

Wysa ni app nyingine nzuri kwa ajili ya Afya ya akili, app hii inakuja na mfumo maalum wa AI ambao utakusaidia kwenye matatizo mbalimbali ya mihemuko na matatizo mengine yanayosababisha sonona (depression). Kupitia app hii utaweza kuchati na mfumo wa AI ambao utaweza kukupa ushauri kwa ajili ya Afya yako.

InnerHour Self-Care Therapy

InnerHour Self-Care Therapy ni app nyingine nzuri ambayo itakusaidia sana kwenye afya yako ya akili, tofauti na app nyingine kwenye list hii app hii itakusaidia kuweza kuwa bora sana kwenye kazi zako za kila siku, app hii itakufundisha jinsi ya kuendana na hali iliyopo pamoja na kukufundisha kujitunza mwenyewe kiakili.

Sanvello

Sanvello ni app nyingine ambayo itakusaidia sana kwenye afya ya akili, app hii ni kama app hizo hapo juu na inakupa uwezo wa kupambana na magonjwa ya sonona na magonjwa mengine ambayo yanasababishwa na afya ya akili. App hii ni nzuri sana na hakikisha unajaribu app hii.

All Mental Disorders and Treatment

App nyingine kwenye list, ni All Mental Disorders and Treatment app hii itakusaidia kujua matatizo mbalimbali ya akili ikiwa pamoja na maana zake. Kama unataka kujua aina mbalimbali za matatizo ya akili ikiwa pamoja na dalili zake kwenye ujumla basi app hii inaweza kukusaidia sana.

Na hizo ndio app nzuri ambazo nimekuandalia siku ya leo, kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua app nyingine nzuri za kujaribu kwenye simu yako kwa sasa. Kwa habari zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use