Njia 4 Bora za Kusaidia Kukumbuka Password Yoyote (2020)

Tumia njia hizi kuweza kupata password zako kama unasahau haraka
Njia 4 Bora za Kusaidia Kukumbuka Password Yoyote (2020) Njia 4 Bora za Kusaidia Kukumbuka Password Yoyote (2020)

Kama wewe ni kama mimi na umekuwa na vitu vingi mtandao kiasi cha kushindwa kukumbuka password za kila kitu basi makala hii ni kwaajili yako. Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ambazo zinaweza kukusaidia kukumbuka password yoyote kwa haraka na urahisi.

Huna haja ya kuwa na ujuzi wowote kitu cha muhimu ni kuwa na smartphone yako na kuwa na Internet ya kuweza kupakua programu kutoka kwenye soko la Play Store au App Store. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye njia hizi.

Njia 4 Bora za Kusaidia Kukumbuka Password Yoyote (2020)

Advertisement

1. Kumbuka Password kwa Tumia LastPass

Lastpass ni app bora ambayo itakusaidia kuweza kuhifadhi password zako kwa urahisi na haraka. App hii itakusaidia kuhifadhi password zako na kuziweka kwenye sehemu ya kujaza password kila wakati unapotaka kuandika password. Yani mbali na kuhifadhi password, app hii itakusaidia kuandika password kwenye kila sehemu ambayo unayotaka kuandika password.

LastPass – Android

LastPass – iOS

2. Kumbuka Password kwa Tumia Dashlane

Dashlane ni app nyingine ambayo itakusaidia sana kukumbuka password kwa haraka, app hii ni kama app iiyotangulia lakini app hii inakupa uweza wa kukumbuka password na kutumia fingerprint kuweza kujaza password yoyote ambayo unataka kuandika mahali popote. Kizuri kuhusu app hii ni kuwa unaweza kuhifadhi password zako kwenye mtandao hivyo hutoweza kuzipoteza tena.

Dashlane – Android

Dashlane – iOS

3. Kumbuka Password kwa Kutumia Keeper

App nyingine ambayo inaweza kukusaidia kukumbuka password yoyote kwa haraka na kwa urahisi nia Keeper. App hii inakuja na uwezo mzuri sana wa kuhifadhi password zako kwenye mpangilio sahihi. Unachotakiwa kufanya ni kupakua app hii kisha tengeneza akaunti na moja kwa moja app hii itaweza kuanza kuhifadhi password yoyote unayotaka kutumia kwenye akaunti yoyote.

Keeper – Android

Keeper – iOS

4. Kumbuka Password kwa Kutumia Enpass

App nyingine ambayo inaweza kukusaidia kukumbuka password zako kwa haraka ni Enpass, app hii ni nzuri sana kwa sababu inakupa urahisi wa kufidha password zako sehemu ambazo unataka wewe, kwa mfano unaweza kuchagua kuhifadhi password zako kwenye akaunti yako ya Google au kupitia sehemu yoyote ambayo una amini kuwa ni rahisi kwako.

Enpass – Android

Enpass – iOS

Na hizo ndio njia nne ambazo unaweza kutumia kukumbuka password yoyote kwa urahisi na haraka. Kumbuka njia hizi haziwezi kukusaidia kukumbuka password kabla ya kuanza kutumia app hizi, ni muhimu kuanza kutumia app hizi kwanza ndipo utaweza kupata password zako zote bila kuwa na haja ya kuzikumbuka kwa namna yoyote.

Pia kumbuka kuwa na password yenye ubora na kwa hilo unaweza kusoma hapa kujua sheria za kuwa na password bora mtandaoni ambayo haiwezi kudukuliwa (Kuwa Hacked) kirahisi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use