in

Zifahamu Hizi Hapa Sheria za Kuwa na Password (Nywila) Bora

Fuata sheria hizi kama unataka kutengeneza password bora

Zifahamu Hizi Hapa Sheria za Kuwa na Password (Nywila) Bora

Kama wewe ni mtumiaji wa huduma mbalimbali mtandaoni basi lazima unayo password au nywila kwenye huduma hizo unazotumia, lakini mbali ya kuwa password ni wazi kuwa watu wachache sana ambao wanajua kuwa kuna sheria muhimu ambazo zinaongo utumiaji wa password ikiwa pamoja na sheria za muhimu za kufuata ili kuwa na password bora.

Kupitia makala hii fupi ya leo ningependa nikujuze sheria angalu kwa uchache, sheria ambazo zinaongoza utumiaji bora wa password ikiwa pamoja na utumiaji bora na sahihi wa password au nywila au neno la siri kama inavyo tambulika na watu wengi hapa Tanzania.

Historia ya Password

Kabla ya yote labda turudi nyuma kidogo hadi miaka ya 1960, ambapo ndio inasemekana kuwa password ya kwanza ya kompyuta ilitumika kwenye chuo cha MIT huko nchini marekani. Inasemekana kuwa kipindi hicho kompyuta zilikuwa haziwezi kufanya kazi ya mtu zaidi ya mmoja hivyo ni lazima watumiaji wasubiri mtu mmoja amalize kazi ndipo mtu mwingine aweze kutumia.

Zifahamu Hizi Hapa Sheria za Kuwa na Password (Nywila) Bora

Swala hilo lilimkasirisha sana mwana sayansi Fernando J. Corbató, ambaye anasemekana kuwa alikuja na mfumo ambao ulikuwa ukiwezesha watumiaji kushirikiana kutumia kompyuta. Hata hivyo tatizo kubwa la usalama lilizaliwa, Fernando J. Corbató aliamua kutengeneza password ili kutenganisha kazi ya mtumiaji mmoja na mwingine, Huo ndio uliokuwa mwanzo wa Password.

Video : Angalia Uzinduzi wa MacBook Mpya Kwa DK 10

Hata hivyo inasemekana kuwa, Password hiyo ya kwanza ya kompyuta kutengenezwa ndio iliyokuwa password ya kwanza kudukuliwa kwani inasemekana mmoja wa wafanyakazi kwenye maabara ya Fernando J. Corbató, aliona kuwa anahitaji muda wa ziada wa kufanya kazi kwenye kompyuta na hatimaye aliamua kuchapisha password zote zilizokuwa zimehitadhiwa kwenye kompyuta hiyo na kutumia password hizo kuingia kwenye kompyuta hiyo.

Sheria za Password

Sasa mbali ya kuwa password ni neno la siri kwa mtu binafsi na wote tunajua kuwa password ni uamuzi wa mtu, lakini upo muongozo au sheria ambazo zinatumika kuongoza baadhi ya sekta kwenye utumiaji bora wa password. Sheria hizi zipo na zinataka sekta za muhimu kama sekta za serikali na sekta za kiteknolojia kufuata sheria hizo bila kukosea hata kidogo.

Zifahamu Hizi Hapa Sheria za Kuwa na Password (Nywila) Bora

Kwa mujibu wa Taasisi ya marekani ya Viwango na Teknolojia, National Institute of Standards and Technology (NIST), zipo sheria ambazo ndio zinatumika sasa kwenye nchi mbalimbali ambazo zinatumika kutoa muongozo wa utumiaji bora wa Password. Sheria hizo ni kama zifuatazo.

 • Password inatakiwa kuwa na tarakimu zisizo pungua 8 kama zitatengenezwa na binadamu.
 • Password inatakiwa kuwa na tarakimu zisizo pungua 6 kama zitatengenezwa na kompyuta.
 • Kiwango cha mwisho cha urefu wa password kinatakiwa kuwa tarakimu 64.
 • Alama moja kwenye alama za All ASCII (ambazo ni pamoja na alama za [email protected]#$%^&*()_+) zinatakiwa kuwekwa pale unapo tengeneza password.
 • Password lazima iwe na namba au herufi kubwa moja ama mbili.
 • Inatakiwa kubadilisha Password yako kila baada ya miezi sita.
 • Password haitakiwi kuwa namba zilizo zoeleka, jina la mtu, mahali au kitu.
 • Hairuhisiwi kukosea password zaidi ya mara 10.
 • Hairuhusiwi kutengeneza password ya muda mfupi, yaani password ambayo inaisha muda wake.
 • Hairuhusiwi kumuonyesha mtu maneno ambayo yatamfanya akumbuke password yake (Password Hint).
 • Hairuhusiwi kushare na mtu yoyote password yako.
Sunday Movie #16 : Movie Nzuri ya Kuangalia Jumapili

Hizi ni baadhi tu ya sheria ambazo zime orozeshwa kwenye nakala hiyo, kama unataka kusoma nakala nzima unaweza kusoma hapa.

Kwa ufupi kabisa password ni kitu cha muhimu na kinatunza mambo mengi sana ambayo mengi ya mambo hayo yakiangukia kwenye mikono ya waalifu uleta madhara makubwa. Ni jukumu lako kutengeneza password bora na kuweka ulinzi wa ziada kwenye huduma unazo tumia ili kuhakikisha unakuwa salama hasa mtandaoni. Pia ni muhimu kutunza password yako mwenyewe na usishiriki password na mtu mwingine yeyote.

Kama unataka kujua jinsi ya kuzuia mtu ku-hack akaunti zako za mitandao ya kijamii, basi unaweza kusoma hapa hatua kwa hatua jinsi ya kulinda akaunti zako za instagram, Facebook na Twitter. Kwa habari zaidi kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.