in

Jifunze Hapa Maujanja Mapya ya WhatsApp 2018 – 2019

Jifunze hapa njia mpya za kutumia programu ya WhatsApp

maujanja ya whatsapp12:52

Najua kuwa asilimia kubwa ya wasomaji wa tovuti hii wanatumia programu ya WhatsApp, na hii ndio sababu leo nimependelea kukujuza kuhusu maujanja haya ya WhatsApp ambayo najua kwa namna moja ama nyingine yanaweza kurahisha maisha yako.

Njia hizi ni rahisi sana kufuata na unahitaji tu kuwa na Internet ili uweze kufanikisha, pia kama unatumia simu ya Android unatakuwa kuwa na bando la kutosha angalau MB 300 kwaajili ya kudownload programu mbalimbali. Kama tayari unalo bando basi twende tukajifunze njia hizi moja kwa moja.

Kama tayari ume angalia video hapo juu basi unaweza kupata Application zote zilizo zungumziwa kwenye maujanja hayo kwa kubofya link ya app husika hapo chini.

  • NotiSave
Notisave
Price: Free

Naoti Save ni app kwaajili ya kukusaidia kusoma meseji ambazo zimefutwa, app hii ni nzuri sana hasa kama unapenda kujua ni kitu gani mtu ameandika pale anapofuta meseji ambayo bado hukufanikiwa kuweza kuisoma. Jinsi ya kutumia app hii angalia video hapo juu.

  • WhatsDirect
Jinsi ya Kuanzisha Podcast kwa Urahisi na Bure (100%)
WhatsDirect - Chat w/o Contact
Price: To be announced

Whats direct ni app ambayo itakusaidia kuweza kutuma meseji ya whatsapp kwa mtu bila hata kuwa na namba yake kwenye simu yako. App hii ni nzuri kama unataka kuwasiliana na mtu mara moja na utaki kusave namba yake kwenye simu yako.

  • Away
WhatAuto - Reply App

Away ni app ambayo itakusaidia kuweza kujibu meseji zako za WhatsApp bila kuandika kwa mkono. App hii inaweza kuwa kukusaidia kutuma meseji pale utakapo kuwa hutaki kushika simu yako kujibu meseji watu kila mara. App hii ni nzuri kwa wafanya biashara ambao hawataki usumbufu wa kushika simu kujibu meseji za wateja kila mara.

  • Audio Status Maker
Audio Status Maker
Price: Free

Kama kwa namna yoyote unataka kuweka status ya muziki ambao hauna video kwenye sehemu ya status kwenye programu yako ya WhatsApp basi app hii ni nzuri sana kwako. App hii inakupa uwezo wa kuweka nyimbo za mp3 kwenye sehemu ya Status ya WhatsApp, wote tunajua kuwa huwezi kuweka audio kwenye status bali ni lazima kuweka video, lakini app hii inakusaidia kuweka audio kwenye sehemu hiyo. Angalia video hapo juu kujifunza zaidi.

Njia Bora ya Kuondoa Background kwenye Picha (Android)

Na hayo ndio maujanja ya WhatsApp niliyo kuandalia kwa siku ya leo, Kama una maswali au kuna mahali ujaelewa unaweza kuuliza swali hapo chini kwenye sehemu ya maoni na sisi tutajitahidi kukujibu kwa wakati. Kwa maujanja zaidi soma hapa, Pia ili kuhakikisha unakuwa wa kwanza kupata maujanja haya kwa njia ya video hakikisha una subscribe kwenye channel yetu ya Tanzania Tech, pia bofya alama ya kengele kwani na kuhakikishia huta jutia alafu pia ni BUREEEE KABISAAA!

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments