in

Zifahamu Sifa na Bei ya Simu Mpya ya BlackBerry Key2

Toleo jingine jipya la simu ya BlackBerry KeyOne

Sifa na Bei ya BlackBerry Key2

Blackberry kupitia kampuni ya TCL, leo imezindua simu yake ya Blackberry Key2 simu ambayo tumeiona kwenye tetesi nyingi za siku za karibuni. Kama tulivyo sema kwenye makala zetu za awali simu hii ni muendelezo wa toleo la Blackberry KeyOne ambayo ilizinduliwa na TCL mwaka jana 2018.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Simu hii ya Blackberry Key2 haina tofauti sana na simu ya mwaka jana, utofauti mkubwa upo kwenye kamera pamoja na kuongezeka kwa ukubwa wa simu hiyo tofauti na simu ya mwaka jana ya KeyOne. Zifuatazo ni sifa kamili na bei ya simu hii ya BlackBerry Key2.

Sifa za BlackBerry Key2

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 4.5 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 1620 pixels, 3:2 ratio (~434 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260), Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 512
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko mbili moja ina GB 64 na nyingine ina GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 8 yenye (f/2.0, 1.12µm), 1080p.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye uwezo wa (f/1.8, 1/2.3″, 1.55µm, DP PDAF) na nyingine ikiwa na Megapixel 12 yenye (f/2.6, 1.0µm, PDAF), huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging) (Quick Charge 3.0).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, 3.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black, Silver.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Mbele).

Bei ya BlackBerry Key2

Simu hii mpya ya BlackBerry Key2 inategemewa kuingia sokoni mwezi huu na inatrajiwa kuuzwa kwa dollar za marekani $649 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1,477,000. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja na kupanda ua kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Zifahamu Sifa na Bei ya Simu Mpya ya BlackBerry Key2
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.