Sifa za Simu Mpya ya BlackBerry KeyOne Iliyozinduliwa Jana

Ulikua unaingoja kwa hamu hii ndio Blackberry KeyOne
BlackBerry Keyone BlackBerry Keyone

Kama wewe ni mpenzi wa simu za blackberry lazima utakua ulikua unajua kwa Blackberry kwa kushirikiana na TLC walifanya uzinduzi wa simu yake mpya ya Blackberry KeyOne, simu hiyo iliyozinduliwa jana huko nchini Barcelona ni moja kati ya simu mpya za mwaka huu zenye kutumia Android kutoka kwa kampuni hiyo ya muda mrefu.

  • Sifa za BlackBerry KeyOne

BlackBerry KeyOne inakuja na uwezo mkubwa wa processor kwani inatumia processor ya snapdragon 2GHz octa-core pamoja na RAM ya GB 3 uku ikiendeshwa na mfumo wa uendeshaji wa Android 7.1 Nougat. Kwa upande wa kioo simu hii inatumia kioo cha inch 4.5 kikiwa na resolution ya 1620×1080 pixels pamoja na ukubwa wa memory ya ndani wa GB 32, kwa upande wa kamera simu hii inatumia kamera ya nyuma yenye Megapixel 12 na ya mbele yenye Megapixel 8 Simu hii inaendeshwa na batter yenye nguvu ya 3505mAh ikiwa na uwezo wa kudumu na chaji karibia siku nzima.

Advertisement

Kingine simu hii inawezesha Touch Screen pamoja na Fingerprint zote zikiwa zinapatikana juu ya keyboard ya simu hiyo, kifupi ni kwamba unaweza kugusa kioo au kutumia keyboard au unaweza kugusa keyboard kama sehemu ya Touchscreen. Simu hii inategemea kuingia sokoni hivi karibuni kwa dollar za marekani $549 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,300,000. Kujua mengine kuhusu simu hiyo endelea kutembelea Tanzania Tech.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembela Tanzania Tech au unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari kwa haraka zaidi, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya youtube ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use