Muonekano wa blackberry-key2

Muonekano wa BlackBerry Key2 Wavuja Kabla ya Uzinduzi

Hivi karibuni, Blackberry ilitangaza kuwa inajiandaa na uzinduzi wa simu yake mpya ya BlackBerry Key2, Simu hii ni mwendelezo wa toleo la Blackberry KeyOne ambayo ilizinduliwa mwaka jana.

Habari mpya hivi karibuni ni kuhusu muonekano wa simu hiyo ya BlackBerry Key2 muonekano ambao umevujishwa mapema kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa simu hiyo. Muonekano huo umevujishwa na mvujishaji maarufu wa mambo ya teknolojia kupitia mtandao wa Twitter anae itwa Evan Blass.

Kwa kuangalia muonekano wa simu hiyo ya BlackBerry Key2 hapo juu, ni wazi simu hiyo haina tofauti sana na toleo lilio pita la simu ya BlackBerry KeyOne. Tofauti kubwa iliyopo kwenye toleo la sasa ni uwepo wa kamera mbili kwa nyuma na kitufe kipya kinacho onekana upande wa kulia chini kwenye keyboard ya simu hiyo.

Mbali na hayo bado hakuna mabadiliko mengine mengi kwa upande wa muonekano wa simu hii, labda tusubiri mpaka tarehe 7 ya mwezi huu ambapo BlackBerry ndio itaenda kuzindua rasmi simu hiyo ya BlackBerry Key2 na Tutakujuza zaidi kuhusu sifa kamili za ndani za simu hiyo bila kusahau na makadirio ya bei yake kwa hapa Tanzania.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
mfumo mpya wa iOS 12
Ujio wa Mfumo wa iOS 12 Haya Hapa Ndio Mabadiliko Mapya
Next Post
macOS Mojave

Fahamu Kuhusu Mfumo Mpya wa Kompyuta wa macOS Mojave