in

Programu 6 Bora za Android za Kuedit Picha Mwaka 2017

Zifuatazo ni programu bora za kuedit picha kwa mwaka huu 2017

kuedit picha

Kama wewe ni mmoja kati ya watu wanaopenda kuedit picha kwa kutumia simu yako ya mkononi ya Android, basi ifuatayo ni list ya programu bora za kuedit picha kwa mwaka huu 2017. Programu zote hizi zinapatikana kupitia soko la mtandaoni la Google Play hivyo jisikie huru kudownload programu hizi wakati wowote utakapo amaua.

Adobe Photoshop Lightroom

Wote tunaijua kampuni ya Adobe ni moja kati ya kampuni inayotengeneza programu bora za kuedit picha za vifaa vyote vya Android, Windows na Pia Mac OS. Programu hii ni bora sana hasa kama unatafuta namna ya kitaalamu zaidi ya kuedit picha zako.

PicsArt Photo Studio

Programu hii ni moja kati ya programu bora sana na inafahamika sana kwa ubora wake wa kutengeneza picha bora sana.

AirBrush: Easy Photo Editor

Hii ni programu nyingine kwaajili ya kuedit picha ambayo ni rahisi kutumia na yenye kutengeneza picha kuwa kwenye ubora tofauti na programu zingine.

Cupslice Photo Editor

Cupslice Photo Editor

Programu hii pia ni moja kati ya programu bora sana za kuedit picha, unaweza kujaribu programu hii kwenye simu yako kisha tupe maoni yako.

Photo Editor by Aviary

Photo Editor by Aviary

Hii ni kati ya programu bora sana za kuedit picha unaweza kujaribu programu hii sasa kwa kuidownload moja kwa moja kwenye simu yako.

Snapseed

Snapseed
Price: Free

Programu hii kutoka kampuni ya Google ni moja kati ya programu bora sana na inauwezo mkubwa sana wa kuedit picha na kuzifanya zivutie.

Kwa habari nyingine za teknolojia endelea kutembelea tanzania tech, na kama una swali unaweza kuuliza kupitia Tanzania Tech Forum.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment