Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Baada ya Kodi ya Mitandao Uganda Kuzuia Tovuti za Ponografia

Tovuti 27 zimetakiwa kufungiwa nchini humo.
Tovuti za Ponografia Uganda Tovuti za Ponografia Uganda

Hivi karibuni serikali ya uganda kupitia mamlaka ya mawasiliano nchini humo ilianzisha kodi mpya kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, kodi ambayo inawataka watumiaji wa mitandao hiyo kulipa shilingi za uganda 200 kwaajili ya kutumia mitandao hiyo.

Sasa baada ya kuanzishwa kwa kodi hiyo, Hivi karibuni mamlaka ya mawasiliano ya nchini humo inasemekana kuanza kufungia tovuti za ponografia kufanya kazi nchini humo. Kwa mujibu wa tovuti ya Quartz, tovuti zaidi ya 27 zinazo onyesha video za ponografia zitafungiwa huku kati ya hizo, tovuti 10 zikiwa ni tovuti kubwa duniani na nyingine 17 zikiwa ni tovuti za nchini humo ambazo kwa mujibu wa Quartz ni tovuti zinazo tangaza huduma za usindikizaji (escort services).

Advertisement

Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti hiyo, Mwaka 2017 Uganda iliunda kamati ya udhibiti wa ponografia ( Pornography Control Committee ) kamati ambayo pia ndio imetoa listi ya tovuti hizo zinazotakiwa kufungiwa nchini humo. Kamati hiyo inaundwa na watu tisa ambao hufanya kazi ya kuchunguza na kuzuia matumizi ya ponografia nchini uganda.

Hata hivyo hadi kufikia siku ya ijumaa iliyopita, kampuni zinazotoa huduma za internet nchini uganda zilikuwa hazijafanya hatua hiyo ya kufungia tovuti hizo kuonekana kuanzia ilipotangazwa hapo tarehe 6 na kupelekea mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Mawasiliano ya Uganda kuwambia waandishi wa habari kuwa, kampuni ambazo hazito tekeleza hatua hiyo zitaadhibiwa kwa kutozingatia masharti hayo.

Kwa mujibu wa Quartz, hadi kufikia siku ya jumatatu asubuhi, baadhi ya kampuni zinazotoa huduma za Internet nchini uganda zilikuwa tayari zimesha anza kutekeleza agizo hilo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use