Kuanzia Leo Waganda Kulipia Matumizi ya Mitandao ya Kijamii

Kuanzia leo wananchi wa uganda kuanza kulipia mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii Uganda Mitandao ya kijamii Uganda

Kama umekuwa mfuatiliaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii, basi lazima utakuwa unajua kuwa bunge la uganda limepitisha sheria ya kuanza kuwalipisha watumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii nchini humo. Mitandao hiyo ni pamoja na Facebook, Twitter, Viber, na WhatsApp.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Quartz Africa, sheria hiyo ilianza kufanyiwa kazi mwezi Aprili baada ya rais wa nchini humo, Yoweri Museveni, kuandika barua kwa hazina ambayo inasema kwamba mitandao ya kijamii inatumika kusambaza uvumi ambayo inapotezea muda na pesa.

Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa leo Julai 1, wananchi wa uganda wanaotumia mitandao ya kijamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 121 kila siku, sawa na makadirio ya Tsh 44,200 kwa mwaka mzima.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use