Waliolipia ving’amuzi Azam, Dstv, Zuku Kurejeshewa Fedha

Ufafanuzi kuhusu kurudishiwa fedha kwa watumiaji wa baadhi ya Ving’amuzi
Vingamuzi vya azam dstv na zuku Vingamuzi vya azam dstv na zuku

Habari kupitia tovuti ya gazeti la mwananchi zinasemakuwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema kampuni zinazotoa huduma za ving’amuzi zinapaswa kuwarejeshea fedha wateja wanaotumia ving’amuzi hivyo kutokana na kukiuka masharti ya leseni.

Kamwelwe amezitaja kampuni hizo kuwa Azam, Dstv na Zuku na kwamba zimekiuka masharti ya leseni zao. Kampuni hizo ziliondoa chaneli za ndani zisizolipiwa baada ya tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), lililokusudia kusimamisha leseni kwa maelezo ya ukiukwaji wa masharti.

Tangazo hilo la TCRA lilieleza kuwa kampuni hizo zimekuwa zikionyesha chaneli zilizopo kwenye orodha ya zile za bure kinyume cha matakwa ya leseni zao ambazo zinaelekeza kuwa wasionyeshe.

Advertisement

UpdateAngalia hapa ufafanuzi uliotolewa na waziri wa habari Tanzania kuhusu kutopatikana kwa chaneli za ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumamosi Agosti 11, 2018 Kamwelwe amesema, “lazima watumiaji walipwe kwa sababu kampuni hizi zina makosa na fedha hizo hazijalipwa serikalini. Subiri tutatoa deadline (muda wa ukomo) wa namna watakavyolipwa watumiaji hawa wa ving’amuzi.”

Waziri Kamwelwe ameongeza akisema, “naona mmetuwahi kutuuliza jambo hili, lakini niwahakikishe TCRA inalifanyika kazi kuhusu urejeshaji huu. Lazima warudishe (fedha) kwa mujibu wa taratibu kwa sababu wamefanya makosa.”

Amesema televisheni za ITV, Clouds, EATV na Channel Ten walitoa maoni kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kadhia hiyo wakiwa na hoja kuwa busara iliyotumika huko nyuma kwa vituo hivyo kupeleka maudhui yao kupitia ving’amuzi vya Azam, Dstv na Zuku iendelee wakati utaratibu wa kurekebisha sheria ukiendelea.

“Jambo la msingi la kujiuliza ni TCRA kuendelea kuangalia sheria na kanuni za utangazaji zikivunjwa kila kukicha au wachukue hatua ili sekta ya habari iendeshwe kwa mujibu wa sheria?” amehoji Kamwelwe.

Kamwelwe ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuzingatia kuwa ni lazima sheria na kanuni za nchi zifuatwe kikamilifu na kila mwenye leseni aiheshimu. Pia, aliwataka wananchi kutumia ving’amuzi sahihi ili kupata huduma za maudhui yasiyo na malipo.

“Ving’amuzi vya Azam, Zuku na Multichoice havijazuiliwa, bali vitaendelea kutumika kwa mujibu wa masharti ya leseni zao,” amesema waziri huyo.

Imenakiliwa Kutoka Tovuti ya Mwananchi, na Kuhaririwa na Tanzania Tech

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use