Hatimaye Google Imezindua Mfumo Mpya wa Android 9 Pie

Baada ya mfumo wa Android Oreo sasa ni mfumo wa Android Pie
Hatimaye Google Imezindua Mfumo Mpya wa Android 9 Pie Hatimaye Google Imezindua Mfumo Mpya wa Android 9 Pie

Baada ya majaribio ya muda mrefu ya mfumo wa Android P, Hatimaye hivi leo kampuni ya Google imezindua rasmi mfumo huo ambao sasa unakuja na jina la Android 9 Pie. Mfumo huu sasa utakuwa unapatika rasmi kwenye simu mbalimbali za Android kama toleo jipya la mfumo wa Android 8 Oreo.

Mfumo huu unakuja na mabadiliko kadhaa ikiwa pamoja na mfumo wa AI au Artificial intelligence kwaajili ya kufanya mambo mbalimbali kwenye simu yako bila wewe kushika simu yako kila mara, baadhi ya mabadiliko hayo ni kama yafuatayo.

  • Adaptive Battery na Adaptive Brightness

Moja ya mabadiliko mapya kwenye mfumo wa Android 9 Pie ni pamoja na sehemu mpya za Adaptive Battery na Adaptive Brightness, sehemu hizi kama jina linavyosema zinahusu zaidi battery pamoja na kioo cha simu yako. Kwenye mfumo huo mpya sehemu ya Adaptive Battery, itasaidia kuweza kutunza chaji zaidi kwenye simu yako kwa kuzuia chaji inayotumiwa na app ambazo hutumi kwa sana kwenye simu yako. Vilevile sehemu ya Adaptive Brightness yenyewe pia itakuwa inapunguza mwanga wa kioo kulingana na eneo ulilopo au app unayotumia.

Advertisement

  • App Actions

Mabadiliko mengine kwenye Android 9 Pie ni sehemu ya App Actions, Sehemu hii ya App Actions itakusaidia kuweza kuonyesha App mbalimbali juu ya kioo cha simu yako kulingana na muda mahali au pale unapofanya jambo fulani. Kwa mfano kama ukichomeka headphone sehemu hiyo inaweza kuonyesha app za muziki juu ya kioo chako ili kukupa uwezo wa kuchagua ni app gani utumie.

  • Overview

Sehemu nyingine kwenye mfumo wa Android 9 Pie ni sehemu mpya ya Overview ambayo mara nyingi inafahamika kama kitufe cha kushoto. Kwenye mfumo huo sehemu ya kitufe cha kushoto imeondolewa na sasa utakacho fanya ili kutoka kwenye app moja kwenda kwenye app nyingine bile kufunga app hiyo ni kupapasa na kidole kwenye kioo cha simu yako kwa kwenda juu au swipe up.

  • Digital Wellbeing

Android 9 Pie, pia inakuja na sehemu mpya ya Digital Wellbeing. Sehemu hii itakusaidia kuweza kuangalia matumizi ya app kwenye simu yako ili kuweza kuzuia uraibu wa utumiaji wa App hizo. Pia sehemu hiyo itaweza kuwasha sehemu ya kuzuia usumbufu (do not disturb) ifikapo wakati wa usiku pamoja na kuwasha Night mode ifikapo muda fulani.

Na hizi ndio baadhi tu ya sehemu mpya kupitia mfumo wa Android 9 Pie, mfumo ambao umetangazwa kuanza kupatikana kuanzia siku ya leo kupitia simu mbambali kama za Google Pixel na baadhi ya simu za Sony Mobile, Xiaomi, HMD Global, Oppo, Vivo, OnePlus na Essential. Kwa wale ambao wanatumia simu zingine za kawaida itakubidi kusubiri mpaka mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2019.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use