Wanafunzi Waunda Mtambo wa Kunasa Matumizi ya Simu Shuleni

Matumizi ya simu shuleni sasa yako mbioni kukomeshwa
simu shuleni simu shuleni

Boris Massesa na Adam Rueben ni wanafunzi wengine wabunifu wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Ilboru mkoani Arusha. Wanafunzi hawa wamekuja na ubunifu mpya ambao utafanya matumizi ya simu kwenye maeneo yasiyotakiwa kuweza kukoma.

Kwa kuanza mtambo huu uliobuniwa na wanafunzi hao utakuwa na lengo moja kubwa la kunasa mawasiliano ya simu ya wanafunzi yanayofanyika ndani ya mazingira ya shule. Wote tunajua shule nyingi hapa Tanzania zinakataza kabisa matumizi ya simu kwenye eneo la shule, sasa licha ya kuwepo kwa sheria hizo bado wanafunzi wamezidi kuwa na tabia ya kutumia simu shuleni kitendo ambacho kimekuwa fursa kwa Boris na Adam.

Boris anasema wazo la kutengeneza mtambo huo liliwajia mwaka jana baada ya kukithiri kwa matumizi ya simu kwa wanafunzi kinyume na sheria za shule zinavyoelekeza. Anasema, “Ni jambo ambalo lilikuwa linatupa shida na kutuumiza vichwa mimi na rafiki yangu ndipo tulipofikia wazo la kutengeneza kitu ambacho kitatambua endapo mawasiliano yatakuwa yanafanyika miongoni mwa wanafunzi ndani ya shule.

Advertisement

Akielezea jinsi mtambo huo unavyofanya kazi, Boris alisema Mtambo huu umeunganishwa na simu za baadhi ya walimu ambao hupelekewa taarifa endapo mawasiliano yoyote yatafanyika bwenini au katika mazingira ambayo mara nyingi wanakuwepo wanafunzi. Mtambo huo umekwenda sambamba na uwepo wa ‘application’ (App) ambayo pia imetengenezwa na vijana hao ikiwa na uwezo wa kunasa na kuhifadhi mawasiliano yote ya simu yaliyo fanyika kutwa nzima kwenye eneo la shule.

Kwa jinsi mtambo huo ulivyotengenezwa una uwezo wa kunasa endapo simu, ujumbe mfupi au matumizi ya internet yatafanyika kwenye simu iliyo katika mazingira husika hata kama imefichwa sehemu gani, mtambo huo hutatoa ishara kuonyesha kuna simu katika eneo hilo. “Mwalimu hatopata ujumbe uliotumwa wala kusikiliza mazungumzo ya kwenye simu ila atapata taarifa kuwa kuna simu na kuanzia hapo ataweza kufuatilia hadi kubaini mahali simu yenyewe ilipo pamoja na mhusika,” anasema Adam.

Licha ya wanafunzi hao kufanya ubunifu huo, maisha yao shuleni yamekuwa sio sawa na mwanzo huku wanafunzi wenzao wakionyesha kutofuraishwa na ugunduzi huo shuleni hapo. Adam anaeleza kuwa wamejikuta wakichukiwa na wanafunzi wenzao kwa kile wanachoamini wameiletea shule teknolojia inayowabana na kuwanyima uhuru wao.

Anasema hasira ya wanafunzi wenzao ilifika mbali kiasi cha kuuficha mtambo huo siku chache kabla ya kuja Dar kwa ajili ya kuonyesha ubunifu huo kwenye maonyesho ya wanasayansi wachanga.

Ndoto ya wanafunzi hao ambao wanasoma mchepuo wa sayansi wakichukua masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu ni kuongeza zaidi ujuzi wao kwenye fani ya ulinzi wa mtandao (cyber security).

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use