Hizi Hapa Simu za Nokia na Bei zake kwa Mwaka (2019)

Hizi hapa ndio sifa pamoja na bei za simu 10 bora za Nokia hadi sasa
Simu bora za Nokia na Bei zake Simu bora za Nokia na Bei zake

Kampuni ya Nokia ni moja kati ya kampuni zilizowahi kufanikiwa sana kwenye miaka ya 90, baada ya ujio wa mfumo wa Android kampuni ya Nokia ilianguka kutokana na kuwepo na ushindani mkubwa sana hasa kutokana na makampuni mbalimbali nayo kuanza kutoa simu zenye mfumo huo wa Android.

Miaka kadhaa baadae kampuni ya Nokia sasa imejiunga na mfumo wa Android na sasa imeanza kuja na simu nzuri ambazo leo nimeona nikuletee hii list ya simu bora za nokia pamoja na bei zake. Kumbuka kwenye list hii nita taja simu za Nokia ambazo tayari zimesha toka na zipo sokoni na unaweza kununua hapa Tanzania au hata nje ya nchi.

Basi baada ya kusema hayo basi moja kwa moja twende tukangalie list hii ya simu bora za Nokia pamoja na bei zake kwa mwaka huu 2019.

Advertisement

10. Nokia 3310

Hizi Hapa Simu za Nokia na Bei zake kwa Mwaka (2019)

Nokia 3310 ni moja kati ya simu bora ya bei nafuu kutoka kampuni ya Nokia, Simu hii ni toleo la maboresho la simu ya zamani, na kama wewe ni mmoja wa watu wanao tafuta simu bora ya Nokia yenye uwezo wa kudumu na chaji na isiyokuwa na mambo mengi basi Nokia 3310 ni simu bora ya kununua.

Sifa za Nokia 3310

 • Mfumo wa Uendeshaji – Nokia OS
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 2.6
 • Kamera ya Mbele – Haina
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 2
 • Ukubwa wa RAM – MB 16
 • Uwezo wa Processor –
 • Uwezo wa Battery – 1200 mAh

Bei ya Nokia 3310

Kwa upande wa bei Nokia 3310 inauzwa kwa kati ya Shilingi za Tanzania Tsh 150,000 hadi Tsh 180,000. Unaweza kupata simu hii kwenye maduka mbalimbali ya simu, pamoja na kwa mawakala wa kampuni ya Nokia.

NUNUA HAPA KWA TSH 109,000

9. Nokia 1

Nokia 1

Nokia 1 ni simu nyingine nzuri kutoka kampuni ya Nokia, Simu hii ni moja kati ya simu za kwanza kabisa kutumia mfumo wa Android Go, pia ni moja kati ya simu za kwanza za Nokia zinazotumia mfumo wa Android. Simu hii ni bora sana kama wewe ni mpenzi wa simu za bei rahisi na kama hitaji kutumia Application nyingi kwenye simu yako.

Sifa za Nokia 1

 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Go Edition)
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 4.5
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 2
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 5
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Uwezo wa Processor – 1.1 GHz,Quad, Mediatek MT6737M
 • Uwezo wa Battery – 2150 mAh

Bei ya Nokia 1

Nokia 1 inapatikana kwa makadirio ya shilingi za Tanzania Tsh 180,000 hadi Tsh 200,000. Unaweza kuipata Nokia 1 kwenye maduka mbalimbali ya simu, pia kwa mawakala wa kampuni ya Nokia.

NUNUA HAPA KWA TSH 155,000

8. Nokia 2.1

 

Nokia 2.1

Nokia 2.1 ni simu nyingine nzuri sana ya Nokia kuwa nayo kwa sasa, Uzuri wa simu hii ni moja kati ya simu yenye sifa nzuri kutoka Nokia, pia ni simu ya bei rahisi. Simu hii inatumia mfumo wa Android One, mfumo ambao unatumiwa kwenye simu mpya za Google Pixel za kampuni ya Google.

Sifa za Nokia 2.1

 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 5
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 8
 • Ukubwa wa RAM – GB 1
 • Ukubwa wa ROM – GB 8
 • Uwezo wa Processor – 1.4 GHz,Quad, Qualcomm MSM8917 Snapdragon 425
 • Uwezo wa Battery – 4000 mAh

Bei ya Nokia 2.1

Nokia 2.1 inapatikana kwa bei ya makadirio kuanzia 250,000 hadi Tsh 300,000. Simu hii inapatikana kwenye maduka mbalimbali pia inapatikana kwa mawakala wa simu za Nokia pamoja na tovuti za mtandaoni.

NUNUA HAPA KWA 260,000

7. Nokia 3.1

Nokia 3.1

Kama ulikuwa unatafuta simu bora ya kununua kutoka kampuni ya Nokia, basi Nokia 3.1 ni simu bora sana kuwa nayo. Simu hii inakuja na kioo kikubwa lakini pia ni moja kati ya simu za Nokia zenye kamera nzuri, simu hii inafaa watu wanapenda simu za kisasa na zenye uwezo wa kati.

Sifa za Nokia 3.1

 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.2
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 8
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
 • Ukubwa wa RAM – GB 2
 • Ukubwa wa ROM – GB 16
 • Uwezo wa Processor – 1.5 GHz,Octa, MediaTek MT6750
 • Uwezo wa Battery – 2990 mAh

Bei ya Nokia 3.1

Kwa upande wa bei ya Nokia 3.1, simu hii utaweza kuipata kwa makadirio ya shilingi za Tanzania Tsh 400,000 hadi Tsh 350,000. Simu hii nayo pia inapatika kwenye maduka mbalimbali ya simu pamoja na mawakala wa simu za Nokia.

NUNUA HAPA KWA TSH 350,000

6. Nokia 5.1 (2018)

Nokia 5

Kama ukitaja list ya simu bora za Nokia ni wazi kwamba huwezi kuacha kuitaja Nokia 5.1 (2018), Simu hii ni nzuri sana na ni moja kati ya simu ambazo zinauwezo mkubwa sana hadi sasa. Simu hii inasifika sana kwa uwezo wake wa kudumu na chaji pia inasemekana simu hii inauwezo wa kupiga picha vizuri sana.

Sifa za Nokia 5.1 (2018)

 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 8
 • Kamera ya Nyuma – Megapixel 13
 • Ukubwa wa RAM – GB 2
 • Ukubwa wa ROM – GB 16
 • Uwezo wa Processor – 1.4 GHz,Octa, MediaTek MT6755S
 • Uwezo wa Battery – 3000 mAh

Bei ya Nokia 5.1 (2018)

Kwa upande wa bei ya Nokia 5.1 (2018), unaweza kuipata kwa Shilingi za kitanzania Tsh 400,000 hadi Tsh 350,000. Simu hii kwa sasa sio maduka yote wanayo hivyo ni muhimu kuitafuta kwa wakala wa uuzaji wa simu za Nokia.

NUNUA HAPA KWA TSH 400,000

5. Nokia 5.1 Plus

Tetesi za Nokia 5.1 Plus au Nokia X5

Nokia 5.1 Plus au Nokia X5 ni moja kati ya simu nzuri na yenye muonekano mzuri kutoka kampuni ya Nokia, Simu hii inakuja na sifa nzuri ambazo na uhakika watu wengi wataenda kuipenda simu hii. Nokia 5.1 Plus inakuja na mfumo wa kamera mbili kwa nyumba pamoja na teknolojia ya AI.

Sifa za Nokia 5.1 Plus

 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo hadi Android 9 (Pie)
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.86
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 8
 • Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ina Megapixel 18 na nyingine Megapixel 5
 • Ukubwa wa RAM – GB 3
 • Ukubwa wa ROM – GB 32
 • Uwezo wa Processor – 2 GHz,Octa, Mediatek MT6771 Helio P60
 • Uwezo wa Battery – 3060 mAh

Bei ya Nokia 5.1 Plus

Kwa upande wa bei Nokia 5.1 Plus inaweza kupatikana kwenye maduka mbalimbali kwa makadirio ya Tsh 500,000 hadi Tsh 400,000. Simu hii kwa sasa bado haijafika nchini Tanzania, hivyo unaweza kuipata simu hii kwenye tovuti mbalimbali kama Amazon pamoja na Ebay.

BADO HAINA OFA

4. Nokia 6.1 (2018)

Nokia 6

Nokia 6.1 ni simu nyingine kali kutoka kampuni ya Nokia, simu hii ni bora kwa sababu ya uwezo wake pamoja na uzuri wake. Simu hii inakuja na RAM kubwa na ROM kubwa pia ni moja kati ya simu nzuri ambayo inaonekana kutumiwa na watu wengi zaidi. Sasa kama wewe ni mtu unaependa simu zenye uwezo mkubwa na ungependa kutumia simu yenye muonekano mzuri basi Nokia 6 ni simu nzuri sana kwako.

Sifa za Nokia 6.1 (2018)

 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo hadi Android 9 (Pie)
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 8
 • Kamera ya Nyuma –  Megapixel 16
 • Ukubwa wa RAM – GB 4
 • Ukubwa wa ROM – GB 64
 • Uwezo wa Processor – 1.4 GHz Octa, Snapdragon 430
 • Uwezo wa Battery – 3000 mAh

Bei ya Nokia 6.1 (2018)

Kwa upande wa bei ya Nokia 6 (2018), unaweza kuipata simu hii kwa bei ya makadirio kati ya Shilingi za Tanzania 600,000 hadi Tsh 500,000.

NUNUA HAPA KWA TSH 600,000

3. Nokia 6.1 Plus

Sifa na Bei ya Nokia X6 (2018)

Ukitaja list ya simu bora za kununua kwa mwaka huu basi Nokia 6.1 Plus au Nokia X6 ni moja kati ya simu ambayo itakuwa kwenye list hiyo. Kampuni ya Nokia imezidu kubadilika na kuendelea kuleta simu zenye muonekano mzuri zaidi ukilinganisha na hapo awali. Nokia 6.1 Plus ni simu ambayo inawafaa watu wanaopenda simu bora zenye uwezo wa kufanya mambo yote vizuri. Nokia 6.1 Plus haina tofauti sana na Nokia 6.1 kwa upande wa sifa ila ni wazi kuwa Nokia 6.1 Plus ni bora hata kwa muonekano.

Sifa za Nokia 6.1 Plus

 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo hadi Android 9 (Pie)
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 8
 • Kamera ya Nyuma –  Megapixel 16
 • Ukubwa wa RAM – GB 4
 • Ukubwa wa ROM – GB 64
 • Uwezo wa Processor – 2.2 GHz Octa, Qualcomm SDM630 Snapdragon 630
 • Uwezo wa Battery – 3000 mAh

Bei ya Nokia 6.1 Plus

Kwa upande wa bei ya Nokia 6.1 Plus, simu hii inakuja ikiwa inauzwa kwa bei ya makadirio kuanzia Tsh 500,000 hadi Tsh 700,000. Simu hii bado haujafika Tanzania ila pengine tutegemee kuiona simu hii siku za karibuni.

BADO HAINA OFA

2. Nokia 7 Plus

Nokia-7-Plus

Hatuwezi kumaliza list hii ya simu bora za Nokia kabla ya kuitaja hapa Nokia 7.1 Plus, simu hii ni bora sana na ni moja kati ya simu ambayo pia inaonyesha kupendwa na watu wengi zaidi. Nokia 7.1 Plus inakuja na kioo kikubwa na pia inakuja na kamera mbili kwa nyuma, Simu hii pia inakuja na uwezo mzuri sana wa kupiga picha za Selfie hivyo kama wewe ni mpenzi wa Selfie hii ndio simu bora kwako.

Sifa za Nokia 7.1 Plus

 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo hadi Android 9 (Pie)
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.0
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 16
 • Kamera ya Nyuma –  Ziko kamera mbili moja ina Megapixel 12 na nyingine Megapixel 13
 • Ukubwa wa RAM – GB 4
 • Ukubwa wa ROM – GB 64
 • Uwezo wa Processor – 2.2 GHz Octa, Qualcomm Snapdragon 660
 • Uwezo wa Battery – 3800mAh

Bei ya Nokia 7.1 Plus

Kwa upande wa bei Nokia 7.1 Plus inakuja ikiwa inauzwa kwa makadirio ya Tsh 700,000 hadi Tsh 500,000. Simu hii bado haijafika hapa Tanzania kwa sasa.

BADO HAINA OFA

1. Nokia 8 Sirocco

Nokia 8

Hadi muda huu wakati makala hii inaenda hewani, Nokia 8 Sirocco ndio simu bora kuliko zote kutoka kampuni ya Nokia. Sio kwa muonekano wake tu, bali hata sifa za simu hii ni bora sana ukilinganisha na simu nyingi kwenye list hii. Nokia 8 Sirocco ndio simu yenye ROM kubwa kuliko simu nyingine za Nokia na ndio simu ya kisasa zaidi kutoka kampuni ya Nokia hadi sasa kabla ya kutoka kwa Nokia 9 hivi karibuni.

Sifa za Nokia 8 Sirocco

 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 Oreo hadi Android 9 (Pie)
 • Ukubwa wa Kioo – Inch 5.5
 • Kamera ya Mbele – Megapixel 5
 • Kamera ya Nyuma –  Ziko kamera mbili moja ina Megapixel 12 na nyingine Megapixel 12
 • Ukubwa wa RAM – GB 6
 • Ukubwa wa ROM – GB 128
 • Uwezo wa Processor – 2.5 GHz Octa, Qualcomm Snapdragon 835
 • Uwezo wa Battery – 3260mAh

Bei ya Nokia 8 Sirocco

Kwa upande wa bei, Nokia 8 Sirocco sio simu ya bei rahisi simu hii inauzwa kwa kati ya Shilingi za Kitanzania 1,000,000 hadi Tsh 850,000. Kwa bahati mbaya hadi sasa simu hii bado haijafika kwa hapa nchini Tanzania.

BADO HAINA OFA

Na hizo ndio simu bora za Nokia kwa mwaka 2019, kumbuka unaweza kuzipata simu hizi kwa bei nafuu zaidi ya ile iliyotajwa kwa kutembelea ukurasa huu kila siku, tutakuwa tunabadilisha bei kulingana na kupanda au kushuka kwa simu huzika hivyo kama umependa simu moja kati ya hizi usiwe na wasiwasi kwani unaweza kuipata kwa bei nafuu.

Vilevile kumbuka kuwa tutakuwa tunaongeza list hii kila simu mpya ya Nokia itakapokuwa inatoka hivyo basi hakikisha una tembelea ukurasa huu mara kwa mara. Ili kujua zaidi kuhusu simu bora endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

13 comments
 1. Maoni* kaka nimeipenda nokia 6.1 plus na 550,000 naweza kuipata phone number 0765415844 au 0712546383

 2. huwa mara nyingi nakuta post za nokia edge ambayo inafanana na S7 edge jee vp kuhusu ujio wake hiyo??

  1. Nadhani hiyo bado haijatoka, ila ni uhakika ikitoka utakuta makala hapa kuhusu simu hiyo.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use