Kampuni ya Motorola Yazindua Simu Mpya za Moto G7 Series

Hizi hapa sifa pamoja na bei za simu mpya za Moto G7
Kampuni ya Motorola Yazindua Simu Mpya za Moto G7 Series Kampuni ya Motorola Yazindua Simu Mpya za Moto G7 Series

Kampuni ya Motorola ambayo sasa inamilikiwa na kampuni ya Lenovo hivi karibuni imezindua simu zake mpya za Moto G7 series. Matoleo ya Simu hizo mpya ni pamoja na Moto G7 yenyewe, Moto G7 Plus, Moto G7 Power pamoja na Moto G7 Play.

Moto G7

Tukianza na Moto G7, Simu hii inakuja kioo cha inch 6.2 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya LTPS IPS LCD, ambacho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2270 pixels. Simu hii inakuja na kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa na Megapixel 5 zote kwa pamoja zikiwa na uwezo wa kuchukua video za 4K pamoja na slowmotion au hyperlapse.

Kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Megapixel 8 ambayo inakuja na teknolojia ya HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p. Sifa nyingine za Moto G7 ni kama zifuatazo.

Advertisement

Sifa za Moto G7

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1080 x 2270 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×1.8 GHz Kryo 250 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 250 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM632 Snapdragon 632 (14 nm).
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – RAM GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/2.3″, 1.55µm, PDAF. Nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote mbili zinasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya Dual-LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh yenye uwezo wa fast charge.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Ceramic Black na Clear White.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Moto G7 Plus

Kwa upande wa Moto G7 Plus simu hii inakuja na sifa zinazo fanana na simu ya Moto G7, lakini utofauti upo kwenye upande wa kamera za simu hii. Kwa mbele Moto G7 Plus inakuja na kamera ya Selfie ya Megapixel 12 ambayo inauwezo wa kuchukua video za 1080p pamoja na AI.

Kwa nyuma Moto G7 Plus inakuja na kamera mbili, moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 5, kamera zote zikiwa na uwezo wa kuchukua video za 4K kama ilivyo simu ya Moto G7. Sifa nyingine za Moto G7 Plus ni kama zifuatazo.

Sifa za Moto G7 Plus

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 1080 x 2270 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×1.8 GHz Kryo 250 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 250 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Octa-core 1.8 GHz Kryo 260.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – RAM GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 12 yenye uwezo wa kurekodi video za 4k.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 16 yenye f/1.7, 1.22um, PDAF, OIS. Nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye f/2.2, depth sensor. Kamera zote mbili zinasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh yenye uwezo wa fast charge na Quick Charge 4, USB Power Delivery 3.0.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Deep Indigo, Viva Red.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Moto G7 Power

Kwa upande wa Moto G7 Power kama ilivyo jina lake simu hii inakuja na uwezo mkubwa wa battery, simu hii inakuja na ukubwa wa battery ya Li-ion yenye uwezo wa 5000 mAh yenye uwezo wa kudumua na chaji siku mbili kwa matumizi ya kawaida.

Mbali na hayo simu hii inakuja na processor pamoja na sifa nyingine kama zilivyo simu za Moto G7 na Moto G7 Plus. Tofauti kubwa iliyopo kwenye simu hii ni battery pamoja na kamera. Moto G7 Power inakuja na kamera moja ya nyuma yenye Megapixel 12 pamoja na kamera ya mbele ya Megapixel 8, kamera ya nyuma ikiwa inakuja na uwezo wa kuchukua video za 4K.

Sifa za Moto G7 Power

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya LTPS IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 720 x 1570 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×1.8 GHz Kryo 250 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 250 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM632 Snapdragon 632 (14 nm).
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu mbili, moja ikiwa na GB 64 na nyingine ikiwa na GB 32 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM GB 4 na nyingine ikiwa na RAM ya GB 4
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 12 yenye f/1.8, 27mm (wide), 1/2.3″, 1.55µm, PDAF. Ikiwa inasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 5000 mAh yenye uwezo wa fast charge.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Ceramic Black, Marine Blue na Iced Violet.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Moto G7 Play

Toleo la mwisho la Moto G7 Play ni toleo la bei rahisi kuliko simu nyingine zilizo tangulia, Simu hii inakuja na sifa zinazo karibiana na simu nyingine zilizo tangulia ila tofauti ipo kubwa ipo kwenye Kioo pamoja na RAM kwani Moto G7 Play inakuja na RAM ya GB 2 na kioo cha inch 5.7.

Simu hii inakuja na kamera ya nyuma ya Megapixel 13 yenye uwezo wa kuchukua video za 4K pamoja na kamera ya mbele ya Megapixel 8 yenye LED Flash.

Sifa za Moto G7 Play

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.7 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16, pamoja na resolution ya 720 x 1570 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×1.8 GHz Kryo 250 Gold & 4×1.8 GHz Kryo 250 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM632 Snapdragon 632 (14 nm).
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 32 zote ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 2
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 yenye uwezo wa kurekodi video za 1080p@30fps.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 yenye f/1.8, 27mm, 1/2.3″, 1.55µm, PDAF. Ikiwa inasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3000 mAh yenye uwezo wa fast charge.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS, USB 2.0, Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Deep indigo, Fine Gold na Starry Black.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, inatumia laini mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka Headphone maarufu kama Headphone Jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).
Moto G7 Play
Moto G7 Play

Na hizo ndio simu mpya za Moto G7, baadhi ya simu hizi zinatarajiwa kupatikana kuanzia mwezi ujao kwenye mabara ya ulaya, amerika ya kazikazini. Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu bei za simu hizi ila tembelea ukurasa huu tutaongeza bei za simu hizi pale tutakapo zipata rasmi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use