Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya ya Nokia 7.1 (2018)

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya Nokia X7 (2018) au Nokia 7.1 Plus
Sifa na bei ya nokia x7 (2018) pic Sifa na bei ya nokia x7 (2018) pic

Kampuni ya Nokia Hivi karibuni imezindua simu mpya ya Nokia 7.1 Plus simu ambayo nchini China inaitwa Nokia X7 (2018), kama wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech lazima unajua kuwa tayari Nokia ilishazindua simu mpya ya Nokia 7.1 siku kadhaa zilizopita. Sasa toleo hili ni toleo la maboresho ya simu hiyo ya Nokia 7.1.

Nokia X7 (2018) au Nokia 7.1 Plus inakuja na kioo cha inch 6.18 chenye resolution ya 1080 x 2280 pixels pamoja na ukingo wa juu maarufu kama notch, kwa mbele simu hiyo inakuja na kamera ya Megapixel 20, huku kwa nyuma simu hiyo ikiwa inakuja na kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 na nyingine ikiwa na Megapixel 13.

Mbali na hayo Nokia X7 (2018) inakuja na processor ya Snapdragon 710 ambayo inasaidiwa na RAM ya kuchagua kati ya GB 4 na GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa kuchagua kati ya GB 64 na GB 128. Mbali na hayo Nokia X7 (2018) inatarajiwa kuja na toleo la Android 8.1 ambalo baadae litaongezewa hadi toleo la Android 9.0 (Pie). Sifa nyingine za Nokia X7 (2018) au Nokia 7.1 Plus ni kama zifuatazo.

Advertisement

Sifa za Nokia X7 (2018)

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.18 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2280 pixels, na uwiano wa 19:9 ratio (~408 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo) inaweza ku-update hadi Android 9 Pie.
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM636 Snapdragon 636 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 616.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 64 na nyingine inakuja na GB 128 zote zikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 400.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili moja ikiwa na RAM ya GB 4 na nyingine ikiwa na GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 20 yenye f/2.0, 0.9µm.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8, 1/2.55″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF, OIS na nyingine ikiwa na Megapixel 13 yenye Huku zote zikiwa zinasadiwa na Zeiss optics, dual-LED dual-tone flash, panorama, na HDR.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3200 mAh battery battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya Type-C 2.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa nne za Dark Blue, Night Red, Magic Night Silver, Night Black.
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Nokia X7 (2018)

Kwa upande wa bei Nokia X7 (2018) inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia jana, bei ya simu hii itakuwa nbi tofauti kulingana na ukubwa wa ndani. Nokia X7 (2018) yenye RAM ya GB 4 na ukubwa wa ndani wa GB 64 itauzwa kwa Yuan ya china CNY 1,700 sawa na Tsh 562,000 bila kodi. Nokia ya RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 64 itauzwa kwa Yuan CNY 2,000 sawa na Tsh 661,000 bila kodi. Nokia X7 (2018) yenye ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 6 itauzwa kwa Yuan CNY 2,500 sawa na Tsh 827,000 bila kodi.

Bei inaweza kuongezeka kwa nchini Tanzania kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika. Kwa sasa unaweza kutoa oda kupitia tovuti ya JD.com ya nchini China.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use